Vipimo vya lori la gesi
Vyanzo vingine vya mafuta
Malori ya Scania yanayotumia gesi hutumia injini za Otto-cycle za lita 9 au lita 13 ambazo hutumia gesi ya methane kama mafuta.
Gesi ya Biomethane huzalishwa kwa kutumia biogesi ili kutoa uchafu kama vile dioksidi ya kaboni, mvuke wa maji na gesi nyingine zinazopatikana kwa viwango vidogo. Hii inasababisha kuzalishwa kwa bidhaa ya gesi safi ya methane ambayo inaweza kutumiwa kama chanzo bora zaidi cha mafuta.
Matumizi ya gesi ya biomethane iliyobanwa
Matangi ya mafuta yanapatikana katika vifurushi vya chupa 4x80L, 4x95L, 4x118L au 4x152L + 4x118L na masafa ya uendeshaji ya hadi kilomita 820. Matangi haya ya mafuta yanapeana pia nafasi nzuri kati ya barabara na chesisi kuliko matangi ya mafuta ya gesi iliyoyeshwa.
Matumizi ya gesi ya biomethane iliyoyeyushwa
Kiwango cha juu cha uzito wa nishati ya gesi iliyoyeyushwa (LNG) inafanya iwe bora zaidi kwa matumizi ya eno na masafa marefu. Matangi ya mafuta yanapatikana kwa ukubwa wa kuanzia lita 400 hadi 1100 yanayotoa masafa ya uendeshaji ya hadi kilomita 1800.
Aina ya injini zinazotumia gesi
Unaweza kuchagua kutoka kwenye aina mbalimbali za vipimo vya dambra, mifumo ya uendeshaji na chesisi. Kwa kutumia aina za injini inayotumia gesi inayolinganishwa kabisa na chaguo zetu za dizeli – hakuna vipimo bora vya injini nyingine ya gesi vilivyoundwa ili kulingana na matumizi ya magari yako.
Unaweza kuchagua kuanzia kwa bendi ya nguvu ya hp 280 hadi 460 kulingana na shughuli yako.
Injini ya lita 9, 280 hp na 340 hp
Aina ya injini inayotumia gesi ya Euro 6 ya silinda 5 ya Scania inaokoa nafasi na uzito bila kuathiri utendaji au gharama ya uendeshaji. Kwa kutumia injini hii ya Otto, tegemea kupata hali bora ya uendeshaji isiyotoa kelele nyingi.
- 260hp / 1,350Nm
- 340hp / 1,600Nm
Injini ya lita 13, 420 hp na 460 hp
Aina ya injini inayotumia gesi ya Euro 6 ya silinda 6 ya Scania inaokoa nafasi na uzito bila kuathiri utendaji au gharama ya uendeshaji. Injini hii ya Otto inatoa hali bora lakini thabiti ya uendeshaji.
- 420hp / 2,100Nm
- 460hp / 2,300Nm
Gundua Malori ya Scania
Wasiliana na muuzaji wako
Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.