Malori yanayotumia gesi
Bidhaa thabiti kwa huduma safi zaidi ya uchukuzi
Aina ya malori yetu yanayotumia gesi yameundwa kwa hali ya juu na uwezo bora wa uendeshaji na matumizi ya kiwango cha chini cha mafuta na masafa ya uendeshaji ya hadi kilomita 1800.
Aina ya malori yetu yanayotumia gesi yanapatikana na dambra za mfululizo wa L/P/G/R/S, kumaanisha kwamba yanaweza kutumika kwa uendeshaji mgumu wa mijini, hadi kwa uendeshaji wa masafa marefu.
Athari iliyopunguzwa zaidi
Si siri kwamba uchukuzi ni chanzo kikuu cha utoaji wa gesi chafu. Lakini kuwa chanzo kikuu pia kunakuja na uwezo wa kuwezesha mapunguzo makubwa.
Uhandisi usio na kifani
Malori yetu yanayotumia gesi yanaleta usawa bora zaidi kati ya utoaji wa gesi kwa kiwango cha chini, nguvu na aina – injini ya gesi ya lita 13 na uwezo wake kamili wa uendeshaji wa masafa marefu, ujenzi na uendeshaji wa mijini, na mfumo bora na tulivu wa uendeshaji hiyo ni injini ya lita 9. Pamoja, zinaweza kutuwezesha kutoa bidhaa safi, zenye utoaji wa gesi chafu kwa kiwango kidogo na zinazofaa zaidi.
Vyanzo vingine vya mafuta
Jambo la kwanza la kusema ni kwamba gesi zote mbili ni methane na chanzo chake kinaweza kuwa gesi asili au gesi ya biomethane inayoweza kutumika tena. Zote zinaweza kutumika sambamba, hatua inayofanya ubadilishaji wowote kutoka kwa moja hadi nyingine uwe ubadilishaji rahisi na wa moja kwa moja. Kipimo kimoja cha nguvu ya gesi iliyoyeyushwa kinachukua nafasi ndogo ya hadi mara tatu zaidi kuliko kipimo kimoja cha nguvu ya gesi iliyobanwa. Yaani, hii inamaanisha gesi ya methane iliyoyeyushwa ni nzito zaidi na kwa hivyo unaweza kupata nishati zaidi kwa gari kuliko ukitumia gesi ya methane iliyobanwa.
Injini zilizowezeshwa
Injini zinazotumia gesi za Scania zinajulikana kwa kuokoa mafuta, trekta ya kawaida isiyo trela kamili inaweza kwenda masafa ya karibu kilomita 1800. Kwa kutumia gesi ya biomethane kwenye matangi, kiwango cha kupunguza utoaji wa gesi ya CO2 ni 50-90%, kawaida ni 80% katika mtazamo wa mfumo wa uendeshaji ikilinganishwa na dizeli ya kawaida. Inawezekana kubadilisha injini zetu zinazotumia gesi ili zitimize sheria kali za kudhibiti kelele kama vile PIEK-standard Quiet Truck katika Bara Ulaya.
Injini zinazotumia gesi ya biomethane zinazookoa mafuta kwa 5% zaidi
Injini zetu mpya za lita 13 zinazotumia gesi ya biomethane sasa zinatoa chaguo thabiti zaidi za injini, na kwa kuzijumuisha na vipengele kutoka kwa mfumo wetu bora zaidi wa uendeshaji, zinaokoa mafuta kwa 5% zaidi ikilinganishwa na injini zetu za zamani.
Maelezo ya kina kuhusu injini inayotumia gesi
Pata maelezo zaidi
Suluhu za huduma
Scania husaidia kukuhakikishia utendakazi wako kwa anuwai ya huduma zinazolenga utendakazi wako mahususi. Chochote kinachoweza kuboresha faida yako, utapata suluhisho la huduma ya Scania ili kuitoa.
Wasiliana nasi
Wasiliana nasi kwa njia unayopenda, tafadhali chagua njia yako hapa chini:
Weka mipangilio ya lori yako
Tumia zana yetu ambayo ni rahisi kutumia ili ubadilishe lori yako upendavyo kwa ajili ya ufanisi na tija bora. Unda lori inayokufaa zaidi!
Ifanye iwe ya Scania.
Tafuta muuzaji aliye karibu nawe
Wasiliana na wauzaji wetu walioidhinishwa kwa maswali yoyote kuhusu bidhaa, huduma au shughuli zetu katika eneo lako. Wasiliana nasi leo kwa msaada na usaidizi wa kitaalamu.
Tafadhali kumbuka kwamba baadhi ya picha ni za mfano na zinaweza kutofautiana na bidhaa halisi.