Kebini ya Crewcab
Hakuna kuathiti
Siku zote tuko tayari kwa yasiyotarajiwa
Msururu wa P wa Scania CrewCab umejaa sehemu muhimu zilizoundwa mahususi kwa ajili ya kazi za dharura, ikizingatia ufanisi wa wafanyakazi na usalama, na bila uathiri wowote wa ubora. Miongoni mwa nyongezeko ni Dirisha za Scania City Safe na mfumo tofauti wa hali ya hewa kwa eneo la wafanyakazi. Kebini ya Scania Crewcab inapatikana katika vipimo viwili vya urefu. Chagua kati ya Crewcab (3265mm) na Crewcab refu (3645mm).
Kebini ya CrewCab ya Scania inatoa unyumbufu usio na kipimo, starehe na usalama. Kebini hii inaweza kubeba hadi abiria wanane, na mpangilio unaonyumbulika wa ndani na sehemu nzuri ya mwanga, huwasaidia wafanyakazi kujiandaa kwa misheni yoyote ya dharura.
DIRISHA SALAMA LA JIJI
Katika hali finyu, inaweza kuwa vigumu kuona vikwazo na watumiaji wa barabara walio hatarini kama vile watembea kwa miguu na waendesha baiskeli pande zote za gari, hasa karibu na kona ya gari upande wa abiria. Dereva anakaa juu na ana mtazamo mzuri wa trafiki mbele.
Dirisha la hiari la usalama wa jijini lililo chini kwenye mlango wa abiria huboresha nafasi ya kutambua watoto, watembea kwa miguu na waendesha baiskeli karibu na lori. Zaidi, sehemu muhimu kama vile upachikaji wa kiti cha dereva, dirisha la upande lililoshukishwa na sehemu kubwa ya kioo, hutoa mwonekano mkubwa zaidi. Dashibodi pia imeshushwa kidogo ili kuboresha mwonekano wa mbele.
Ufikivu rahisi
Lengo la CrewCab ni kufanya kuingia na kutoka kuwe kwa haraka na salama iwezekanavyo. Kiingilio cha kebini ni cha chini, na vishikizo vinavyofaa vinavyorahisisha kupanda na kutoka. Bodi ya nyuma inayofanana na ngazi huja ikiwa ya kudumu au inayoweza kurudishwa ndani, hivyo basi inawezesha kuingia na kutoka kwa haraka na salama.
ENEO LA WAFANYAKAZI LENYE KUNYUMBULIKA
Scania CrewCab inatoa aina mbalimbali za uwezekano wa kuketi na kuhifadhi vitu kwa wafanyakazi wote. Chaguo sasa zinajumuisha viti vitatu au vinne vya kibinafsi au kiti cha benchi. Viti visivyo na sehemu ya kuegemea pia vinapatikana, ili kutoa nafasi ya kuweka vifaa kama vile vifaa vya kupumua.
Wakati wa ustawishaji wa Scania CrewCab, hali njema ya wafanyakazi imepewa kipau mbele. Mfumo tofauti wa hali ya hewa na ina ukanzaji wake sasa unapatikana kwa eneo la wafanyakazi. Inakaa nyuma ya dereva na ina matundu ya hewa ambayo huelekeza hewa yenye joto kwenye sakafu na kwa madirisha ya kando.
NAFASI YA ZAIDI
Kuwa na nafasi ya vifaa muhimu ni muhimu katika kazi yoyote ya dharura. Kebini ya CrewCab inatoa aina mbalimbali za uwezekano wa kuhifadhi ambapo wafanyakazi wanaweza kuhifadhi gia muhimu. Nafasi nzuri ya kuhifadhi mizigo inaweza kufikiwa kutoka ndani na nje ya kebini. Inapatikana ya CrewCab refu
Kebini ya Crewcab
CrewCab nzuri na inayoweza kubadilishwa na ambayo inaweza kunyumbulika sana na ni rahisi kwa mahitaji yako maalumu.
Kimo
2920 mm (bila vikengeusha vya hewa), Viti: Viti 2 vya mbela na viti vya nyuma hadi 4
Kitanda
Hapana
Mitambo ya injini
220-500 hp
Kebini ya Crewcab ndefu
Kebini ndefu ya CrewCab ina mazingira mazuri na inatoa nafasi ya ziada kwa wafanyakazi wako.
Kimo
2920 mm (bila vikengeusha vya hewa), Viti: Uwezekano wa kuketi hadi watu wanane
Kitanda
Hapana
Mitambo ya injini
220-500 hp
Utiririshaji wa hewa ulioboreshwa
Mbele, paa, upande, chini - maeneo yote yamechanganuliwa, yameundwa na kuboreshwa ili kufikia uvutaji wa hewa wa chini kabisa. Sura ya kebini na pembe zake, mapengo na pembe zote zimepunguzwa na kurahisishwa ili kufikia mtiririko wa hewa wa ufanisi zaidi na mtiririko wa nguvu wa mistari.
MIFUKO YA HEWA YA WAKATI GARI LIMEBINGIRIA
Kebini za Scania za CrewCab zinaweza kuwekwa mifuko ya hewa ya upande wa pazia za wakati gari limebingiria, mfumo wa usalama uliounganishwa kwenye dari. Mifuko ya hewa ya wakati gari limebingiria hulenga mojawapo ya matokeo mabaya zaidi ya ajali za kubingiria, ambapo madereva au abiria hujeruhiwa katika mgongano au kubondwa vibaya hadu kufa na gari lao.
Bidhaa zetu mbali mbali
Wasiliana na muuzaji wako
Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.