You seem to be located in .

Go to your Scania market site for more information.

Vipimo vya magari ya R-series

Yameboreshwa kwa ajili ya kazi yako

Yamebuniwa ili kufaa

Jina la Scania linakuhakikishia matumizi bora zaidi ya mafuta, lakini si hayo tu. Toleo hili la malori yenye Mfumo bora zaidi wa uendeshaji, litakuokolea asilimia kadhaa ya matumizi ya mafuta.

Injini zilizowezeshwa

Injini za magari ya Scania zinajulikana kwa matumizi bora ya mafuta. Injini bunifu ya Super ya lita 13 ya Scania inaboresha zaidi sifa hizo. Kwa utendaji wa injini ulioboreshwa na udhibiti bora zaidi wa utoaji wa gesi ya kaboni kupitia mfumo wa Twin-SCR wa Scania, injini bunifu ya Super ya lita 13 ya Scania inaweka kiwango kipya cha sekta cha ubora wa usambazaji wa nishati ya breki. Hali hii inachangia kiwango cha juu zaidi cha 8% cha kuokoa mafuta ya mfumo wa uendeshaji.

UDHIBITI MARA MBILI WA UTOAJI WA GESI YA KABONI

Mfumo bora zaidi wa Twin-SCR wa Scania, wenye usambazaji mara mbili wa AdBlue, huhakikisha kiwango cha juu cha kuendelea kupunguza utoaji wa gesi ya kaboni katika kazi mbalimbali na uko tayari kutimiza hata sheria kali zaidi za utoaji wa gesi ya kaboni – kwa sasa na siku za usoni.

UTENDAJI WA HALI YA JUU

Mipini miwili yenye kemu iliyowekwa juu ya silinda za ndani ya injini, imewekwa ili kuboresha ubadilishanaji wa gesi na kutoa utendaji bora zaidi. Pamoja na maboresho makubwa ya utendaji wa injini ya mwako wa ndani, ulainishaji na upozaji na utendaji mwingine wa chaja kuu, injini bunifu ya Super ya lita 13 ya Scania inaweka viwango vipya zaidi vya ubora wa usambazaji wa nishati ya breki.

MFUMO THABITI WA BREKI

Kupitia mfumo wa breki wa ziada wa kuachilia mbano, injini bunifu ya Super ya lita 13 ya Scania inasababisha utendaji wa kiwango cha juu, uwezo wa mfumo wa ziada wa breki wa hadi 350 kW – hatua ambayo inahakikisha uendeshaji bora na salama zaidi katika mandhari magumu.

Boresha faida yako

Scania ina aina mbalimbali za injini ambazo zinatumia dizeli na mafuta mbadala, kwa hivyo unaweza kupata mafuta bora zaidi ya kudumisha shughuli zako za masafa marefu, maili baada ya maili. Hii inajumuisha injini mpya bunifu ya Super ya lita 13 ya Scania ambayo inaleta hatua mpya ya utendaji ya 560 hp, kando na kiwango cha juu zaidi cha 8% cha kuokoa mafuta ya mfumo wa uendeshaji.

Nguvu inayotolewa Toki Mafuta Teknolojia ya uchafuzi PTO ya injini
770 Hp 3700 Nm Dizeli/HVO Selective Catalytic Reduction (SCR) 800 Nm
660 Hp 3300 Nm Dizeli/HVO Selective Catalytic Reduction (SCR) 800Nm
590 Hp 3050 Nm Biodizeli/Dizeli/HVO Selective Catalytic Reduction (SCR) 800Nm
530 hp 2800 Nm Dizeli/HVO Selective Catalytic Reduction (SCR) 800Nm

Nguvu inayotolewa Toki Mafuta Teknolojia ya uchafuzi PTO ya injini
560 Hp 2800 Nm Dizeli/HVO SCR Mbili Hadi 1000 Nm
500 Hp 2650 Nm Dizeli/HVO/FAME SCR Mbili Hadi 1000 Nm
460 Hp 2500 Nm Dizeli/HVO/FAME SCR Mbili Hadi 1000 Nm
420 Hp 2300 Nm Dizeli/HVO SCR Mbili Hadi 1000 Nm

Nguvu inayotolewa Toki Mafuta Teknolojia ya uchafuzi PTO ya injini
540 Hp 2700 Nm Dizeli/HVO Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
500 Hp 2550  Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
450 Hp 2350 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
410 Hp 2150 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
410 Hp 2000 Nm GESI Kurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR) 600 Nm
370 Hp 1900 Nm Dizeli/HVO Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm

Nguvu inayotolewa Toki Mafuta Teknolojia ya uchafuzi PTO ya injini
360 Hp 1700 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
340 Hp 1600 Nm GESI Kurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR) 600 Nm
320 Hp 1600 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
280 Hp 1400 Nm Dizeli/HVO Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
280 Hp 1350 Nm GESI Kurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR) 600 Nm

Nguvu inayotolewa Toki Mafuta Teknolojia ya uchafuzi PTO ya injini
620 Hp 3000 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 800 Nm
520 Hp 2700 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 800Nm

Nguvu inayotolewa Toki Mafuta Teknolojia ya uchafuzi PTO ya injini
540 Hp 2700 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
500 Hp 2550  Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
450 Hp 2350 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
440 Hp 2300 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
410 Hp 2150 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
380 Hp 1975 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm

Nguvu inayotolewa Toki Mafuta Teknolojia ya uchafuzi PTO ya injini
360 Hp 1700 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
320 Hp 1600 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli
Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
280 Hp 1400 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm

Nguvu inayotolewa Toki Mafuta Teknolojia ya uchafuzi PTO ya injini
620 Hp 3000 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 800 Nm
520 Hp 2700 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 800Nm

Nguvu inayotolewa Toki Mafuta Teknolojia ya uchafuzi PTO ya injini
500 Hp 2550  Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
450 Hp 2350 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
440 Hp 2300 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
410 Hp 2150 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
380 Hp 1975 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm

Nguvu inayotolewa Toki Mafuta Teknolojia ya uchafuzi PTO ya injini
360 Hp 1700 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
320 Hp 1600 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli
Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm
280 Hp 1400 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Selective Catalytic Reduction (SCR) 600 Nm

Nguvu inayotolewa Toki Mafuta Teknolojia ya uchafuzi PTO ya injini
560 Hp 2700 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Bila SCR 800 Nm

Nguvu inayotolewa Toki Mafuta Teknolojia ya uchafuzi PTO ya injini
460 Hp 2250 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Bila SCR 600 Nm
410 Hp 2050 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Bila SCR 600 Nm
360 Hp 1800 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Bila SCR 600 Nm

Nguvu inayotolewa Toki Mafuta Teknolojia ya uchafuzi PTO ya injini
310 Hp 1550 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli Bila SCR 600 Nm
250 Hp 1250 Nm Dizeli/HVO/Biodizeli
Bila SCR 600 Nm

Pata giaboksi sahihi

Aina mbalimbali za giaboksi zetu zinaweza kubadilishwa ili kutumika kwenye aina zote za shughuli za usafiri ili kutoa usambazaji kamili wa nishati kwenye mfumo wote wa uendeshaji wa gari lako la Scania. Zikiwa zinatoa hali iliyoboreshwa ya uendeshaji, giaboksi za Scania zinaweza kuwekwa na Kidhibiti Mwendo cha Scania cha utendaji wa juu. 

 

Mfumo wa Kubadilidha Gia Kiotomatiki wa Scania wa G25 na G33 unatoa utendaji wa kiwango cha juu zaidi wa giaboksi. Pamoja na uthabiti wa jumla ulioboreshwa, Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania unabaki kuwa chaguo bora zaidi kwa shughuli za kudumu na za kuokoa mafuta za usafiri.

Gia 8

Ubora wa giaboksi hii unapatikana katika urahisi wake. Zikiwa thabiti na imara, hakuna uwiano wa gia na utendakazi bora na laini unafanya iwe rahisi kubadilisha gia. Chaguo zinajumuisha Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania, Kidhibiti Mwendo cha Scania na aina mahususi za mifumo ya usambazaji wa nishati.

Gia 8+1

Giaboksi hii inatoa manufaa sawa, pamoja na uwiano wa ziada wa gia. Kulingana na giaboksi ya kasi 4, pamoja na mipini ya kuingiza na kutoa nishati iliyolinganishwa, nguvu zake haziwezi kulinganishwa na nguvu za kiwango cha juu za uzungushaji za injini yoyote ya ndani ya Scania. Chaguo zinajumuisha Kidhibiti Mwendo cha Scania na aina mahususi za mifumo ya usambazaji wa nishati.

Gia 12

Giaboksi hii imebuniwa ili kukabiliana na mandhari magumu zaidi, hali ambayo inafanya iwe chaguo bora zaidi kwa safari ya masafa marefu zaidi. Uwiano wake wa karibu zaidi wa gia unaunganisha wepesi na urahisi wa uendeshaji na gharama ya chini zaidi ya matumizi.

Gia 12+2

Kwa shughuli ambazo zinahitaji kasi ya chini zaidi ya uendeshaji, giaboksi hii ina gia mbili ziada. Ikiwa imebuniwa ili kupunguza gharama za matumizi, imethibitishwa kuwa fanisi zaidi kwa usafiri wa masafa ya mbali na ya karibu, pamoja na kwa kazi nzito za ujenzi. Gia za kupunguza kasi ya injini zinatoa uwezo wa juu wa nguvu za kuzungusha, pamoja na kupunguza kasi ya mizunguko ya chini na ya kupunguza gharama. Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania na Kidhibiti Mwendo cha Scania, pamoja na aina mahususi za mifumo ya usambazaji wa nishati, inapatikana kwa ajili ya giaboksi zote za kugawanya gia.

Mfumo wa giaboksi ya Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania, ambao unapatikana katika hatua mbili za utendaji za G25 na G33, unatoa huduma iliyoboreshwa na ya haraka ya ubadilishaji wa gia pamoja na starehe bora zaidi na punguzo la matumizi ya mafuta la asilimia moja.

 

Kidhibiti cha klachi cha kiotomatiki cha Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki, ambacho kinaruhusu usahihi wa uendeshaji na utendaji bora wa gia, kinasaidiwa na mfumo mpana na bora zaidi wa gia 14 na teknolojia mpya kama vile kiwango cha oili kinachobadilika na kifaa cha kunyunyiza oili ili kuboresha ulainishaji wa gia na kupunguza hasara za ndani.

 

Mfumo pia una muundo mpya na thabiti wa kijiometri, pamoja na kifuniko chepesi cha aluminiamu, hali ambayo inapunguza zaidi viwango vya sauti na uzito wa kifaa wa hadi kilogramu 75. Pia, Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki unasaidia gari kutumika kwa muda mrefu na mara chache za kufanyiwa matengenezo kupitia vipindi virefu vilivyowekwa kabla ya ubadilishaji wa oili. Hatua hizi zote ni za kuhakikisha kuwa gharama yako ya jumla ya matumizi imepunguzwa.

Giaboksi mpya ya G33 ya Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania inapatikana kwa ajili ya injini zote za V8 za hadi 660 hp pamoja na injini za utoaji wa nishati ya kiwango za lita 13 za hp 500 na 540.

Gia za ekseli ya nyuma

Kampuni ya Scania inatoa aina mbalimbali za ekseli za kuendesha za mfumo mmoja wa kudhibiti kasi. Ekseli ya mfumo wa upunguzaji wa kasi pia inapatikana katika viwango viwilii. Ekseli ya R756 ambayo ni thabiti na nyepesi inatoa huduma bora na ya haraka ya kubadilisha gia, ambayo inaweka viwango vipya vya utendaji wa ekseli ya nyuma na kutoa utendaji ulioboreshwa wa mfumo wa uendeshaji wa Scania.

Ekseli ya kuendesha hebu yenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi

Ekseli za kuendesha hebu zenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi zinapatikana kwa ajili ya shughuli ambazo uwezo wa kuwashwa, nafasi kati ya fremu ya gari na barabara na kiwango cha juu zaidi cha uzito wa gari unaoruhusiwa vinafaa. Hudhibiti kiwango cha juu zaidi cha uzito wa gari kinachoruhusiwa cha hadi tani 80 na uwiano wa gia wa kuanzia 3.80 hadi 7.18.

Ekseli moja ya kuendesha yenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi

Gia zetu za kifaa kimoja cha kupunguza kasi zina kiwango cha chini cha mbano na utendaji wa kiwango cha juu na zinaweza kudhibiti kiwango cha juu zaidi cha uzito wa gari unaoruhusiwa wa hadi tani 78 na uwiano mkubwa wa gia kuanzia 1.95 hadi 5.57.

EKSELI MBILI ZA KUENDESHA ZENYE KIFAA KIMOJA CHA KUPUNGUZA KASI

Ekseli mbili za kuendesha zenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi zinatolewa kwa shughuli ambazo unahitaji kuvuta mizigo na matumizi ya kiwango cha chini cha mafuta. Gia ya kushuka ya RB662 + R660 hudhibiti kiwango cha juu zaidi cha uzito wa gari unaoruhusiwa wa hadi tani 80 na uwiano wa gia wa kuanzia 2.92 hadi 4.88.

Ekseli mbili za kuendesha hebu zenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi

Aina zetu nyingi za ekseli mbili za kuendesha hebu zenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi ni thabiti na za kudumu na zinatoa huduma bora zaidi ya kuwashwa kwa injini na nafasi kubwa kati ya fremu ya gari na barabara. Hudhibiti kiwango cha juu sana cha uzito wa gari unaoruhusiwa wa hadi tani 210 na uwiano wa gia wa kuanzia 3.52 hadi 7.63.

UWIANO MPANA WA GIA

Ekseli ya R756 inatoa uwiano mpana wa gia kuanzia 1.95 hadi 4.11 na imebuniwa kudhibiti uzito mkubwa wa gari wa hadi tani 53 GTW.Info point 2 (+ on image)

WAKATI WA UTENDAKAZI USIO NA USHINDANI

The R756 is engineered to deliver extended oil change intervals and an increased component lifetime.

Mpangilio wa ekseli

Ekseli ya mbele, nyuma, isiyozunguka na inayozunguka – Scania inaweza kutimiza mahitaji ya shughuli yoyote. Magari ya R-series yanaweza kuwekewa aina mbalimbali za fremu zenye urefu tofauti.

4x2
Kimo cha chesisi
Chini zaidi, chini, kawaida, juu

4x4

Kimo cha chesisi
High

6x2
Kimo cha chesisi
Kawaida

6x2/2
Kimo cha chesisi
Kawaida

6x2 ya kusukuma

6x2/4

Kimo cha chesisi
Kawaida, fupi
6x2 inaendeshwa na ekseli mbili

6x4
Kimo cha chesisi
Kawaida, refu

6x6
Kimo cha chesisi
High

4x2
Kimo cha chesisi
Chini, kawaida, juu

4x4
Kimo cha chesisi
High

6x2
Kimo cha chesisi
Fupi, kawaida

6x2/2
Kimo cha chesisi
Kawaida

6x2 ya kusukuma

6x2/4

Kimo cha chesisi
Kawaida
6x2 inaendeshwa na ekseli mbili

6x2*4

Kimo cha chesisi
Fupi, kawaida

6x4
Kimo cha chesisi
Kawaida, refu

6x6
Kimo cha chesisi
High

8x2
Kimo cha chesisi
Kawaida

8x2*6

Kimo cha chesisi
Fupi, kawaida

8x2 inaendeshwa na ekseli ya nyuma

8x2/4

Kimo cha chesisi
Kawaida

8x2 inaendeshwa na ekseli mbili

8x4

Kimo cha chesisi
Kawaida, refu

8x4*4

Kimo cha chesisi
Kawaida

8x4 inaendeshwa na ekseli ya nyuma

10x4*6

Kimo cha chesisi
Kawaida

10x4 inaendeshwa na ekseli ya nyuma

Wasiliana na muuzaji wako

Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.

Call us
E-mail us
E-mail Workshop
View Dealer Website
OPENING HOURS
ACCEPTED CREDIT CARDS

Bidhaa zetu mbali mbali