Vipimo kamili vya mfululizo wa S
Tukufu. Imara. Imehakikishiwa.
Injini zilizowezeshwa
Lori zetu zenye nguvu na zisizotumia mafuta zina umaarufu mwingi. Mfululizo wa S unaimarisha hili zaidi. Aina nzima ya injini za mfululizo wa S hutoa udhibiti wa uzalishaji wa SCR-pekee, na mfumo unaoongoza wa Scania Twin-SCR sasa unapatikana kwenye safu ya hivi karibuni ya injini ya lita 13 na 16 - kupunguza athari za mazingira na matumizi ya mafuta bila kuathiri nguvu. Kuweka gia ni rahisi na haraka zaidi kuliko awali.
Lita 13
Aina zote za injini za Scania za Euro 6 zimeidhinishwa kutumia hadi 100% ya HVO. Ikiwa imetengenezwa kulingana na falsafa ya idadi ya chini ya mizunguko ya chapa ya Scania, Injini bunifu ya Super ya lita 13 ya Scania inakuokolea zaidi matumizi ya mafuta na kukupa utendaji bora zaidi wa injini.
Injini zetu za lita 13 za silinda sita zina viwango vya utoaji wa nishati vya hp 370, 410, 450, 500 na 540 kwa kutumia teknolojia ya SCR.
Lita-13 SUPER
Ikiwa una uwezo wa kiwango cha juu zaidi cha 8% wa kuokoa mafuta ya mfumo wa uendeshaji, pamoja na usambazaji wa nishati, nguvu na uthabiti ulioboreshwa, Injini bunifu ya Super ya lita 13 ya Scania haihakikishi tu utendaji bora na kuwa mashine inatumika kwa muda mrefu, lakini pia iko tayari kutimiza masharti makali zaidi ya kudhibiti utoaji wa gesi ya kaboni kwa sasa na siku za usoni.
Injini zetu Kubwa Zaidi za lita 13 za silinda sita zina viwango vya utoaji wa nishati vya hp 420, 460, 500 na 560.
Lita 16
Injini zote za Euro 6 zimeidhinishwa kufanya kazi kwa hadi 100% ya HVO. Tumepunguza matumizi yake ya mafuta ili kupunguza gharama zako zaidi. Lakini hatuwachia hapo. Tutaendelea kufanya kazi ili kuboresha utendaji kazi ili biashara yako inufaike hata zaidi.
Magari ya Scania V8 yanapatikana na viwango vya nishati vya hp 530, 590, 660 na 770.
Imechochewa na mageuzi
Injini za magari ya Scania zinajulikana kwa matumizi bora ya mafuta. Injini bunifu ya Super ya lita 13 ya Scania inaboresha zaidi sifa hizo. Kwa utendaji wa injini ulioboreshwa na udhibiti bora zaidi wa utoaji wa gesi ya kaboni kupitia mfumo wa Twin-SCR wa Scania, injini bunifu ya Super ya lita 13 ya Scania inaweka kiwango kipya cha sekta cha ubora wa usambazaji wa nishati ya breki. Hali hii inachangia kiwango cha juu zaidi cha 8% cha kuokoa mafuta ya mfumo wa uendeshaji.
UDHIBITI MARA MBILI WA UTOAJI WA GESI YA KABONI
Mfumo bora zaidi wa Twin-SCR wa Scania, wenye usambazaji mara mbili wa AdBlue, huhakikisha kiwango cha juu cha kuendelea kupunguza utoaji wa gesi ya kaboni katika kazi mbalimbali na uko tayari kutimiza hata sheria kali zaidi za utoaji wa gesi ya kaboni – kwa sasa na siku za usoni.
UTENDAJI WA HALI YA JUU
Mipini miwili yenye kemu iliyowekwa juu ya silinda za ndani ya injini, imewekwa ili kuboresha ubadilishanaji wa gesi na kutoa utendaji bora zaidi. Pamoja na maboresho makubwa ya utendaji wa injini ya mwako wa ndani, ulainishaji na upozaji na utendaji mwingine wa chaja kuu, injini bunifu ya Super ya lita 13 ya Scania inaweka viwango vipya zaidi vya ubora wa usambazaji wa nishati ya breki.
MFUMO THABITI WA BREKI
Kupitia mfumo wa breki wa ziada wa kuachilia mbano, injini bunifu ya Super ya lita 13 ya Scania inasababisha utendaji wa kiwango cha juu, uwezo wa mfumo wa ziada wa breki wa hadi 350 kW – hatua ambayo inahakikisha uendeshaji bora na salama zaidi katika mandhari magumu.
Boresha faida yako
Scania ina aina mbalimbali za injini ambazo zinatumia dizeli na mafuta mbadala, kwa hivyo unaweza kupata mafuta bora zaidi ya kudumisha shughuli zako za masafa marefu, maili baada ya maili. Hii inajumuisha injini mpya bunifu ya Super ya lita 13 ya Scania ambayo inaleta hatua mpya ya utendaji ya 560 hp, kando na kiwango cha juu zaidi cha 8% cha kuokoa mafuta ya mfumo wa uendeshaji.
- Euro 6
- Euro 5
- Euro 4
- Euro 3
| Nguvu inayotolewa | Toki | Mafuta | Teknolojia ya uchafuzi | PTO ya injini |
|---|---|---|---|---|
| 770 Hp | 3700 Nm | Dizeli/HVO | Selective Catalytic Reduction (SCR) | 800 Nm |
| 660 Hp | 3300 Nm | Dizeli/HVO | Selective Catalytic Reduction (SCR) | 800Nm |
| 650 Hp | 3300 Nm | Dizeli/HVO | Selective Catalytic Reduction (SCR) | 800Nm |
| 590 Hp | 3050 Nm | Biodizeli/Dizeli/HVO | Selective Catalytic Reduction (SCR) | 800Nm |
| 580 Hp | 3000 Nm | Biodizeli/Dizeli/HVO | Selective Catalytic Reduction (SCR) | 800Nm |
| 530 hp | 2800 Nm | Dizeli/HVO | Selective Catalytic Reduction (SCR) | 800Nm |
| 520 hp | 2700 Nm | Dizeli/HVO | Selective Catalytic Reduction (SCR) | 800Nm |
| Nguvu inayotolewa | Toki | Mafuta | Teknolojia ya uchafuzi | PTO ya injini |
|---|---|---|---|---|
| 560 Hp | 2800 Nm | Dizeli/HVO | SCR Mbili | Hadi 1000 Nm |
| 500 Hp | 2650 Nm | Dizeli/HVO/FAME | SCR Mbili | Hadi 1000 Nm |
| 460 Hp | 2500 Nm | Dizeli/HVO/FAME | SCR Mbili | Hadi 1000 Nm |
| 420 Hp | 2300 Nm | Dizeli/HVO | SCR Mbili | Hadi 1000 Nm |
| Nguvu inayotolewa | Toki | Mafuta | Teknolojia ya uchafuzi | PTO ya injini |
|---|---|---|---|---|
| 540 Hp | 2700 Nm | Dizeli/HVO | Selective Catalytic Reduction (SCR) | 600 Nm |
| 500 Hp | 2550 Nm | Dizeli/HVO/Biodizeli | Selective Catalytic Reduction (SCR) | 600 Nm |
| 450 Hp | 2350 Nm | Dizeli/HVO/Biodizeli | Selective Catalytic Reduction (SCR) | 600 Nm |
| 410 Hp | 2150 Nm | Dizeli/HVO/Biodizeli | Selective Catalytic Reduction (SCR) | 600 Nm |
| 370 Hp | 1900 Nm | Dizeli/HVO | Selective Catalytic Reduction (SCR) | 600 Nm |
Pata giaboksi sahihi
Aina mbalimbali za giaboksi zetu zinaweza kubadilishwa ili kutumika kwenye aina zote za shughuli za usafiri ili kutoa usambazaji kamili wa nishati kwenye mfumo wote wa uendeshaji wa gari lako la Scania. Zikiwa zinatoa hali iliyoboreshwa ya uendeshaji, giaboksi za Scania zinaweza kuwekwa na Kidhibiti Mwendo cha Scania cha utendaji wa juu.
Mfumo wa Kubadilidha Gia Kiotomatiki wa Scania wa G25 na G33 unatoa utendaji wa kiwango cha juu zaidi wa giaboksi. Pamoja na uthabiti wa jumla ulioboreshwa, Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania unabaki kuwa chaguo bora zaidi kwa shughuli za kudumu na za kuokoa mafuta za usafiri.
- Upeo- badilisha giaboksi
- Upeo- kipasua giaboksi
- Giaboksi ya Opticruise
Gia 8
Ubora wa giaboksi hii unapatikana katika urahisi wake. Zikiwa thabiti na imara, hakuna uwiano wa gia na utendakazi bora na laini unafanya iwe rahisi kubadilisha gia. Chaguo zinajumuisha Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania, Kidhibiti Mwendo cha Scania na aina mahususi za mifumo ya usambazaji wa nishati.
Gia 8+1
Giaboksi hii inatoa manufaa sawa, pamoja na uwiano wa ziada wa gia. Kulingana na giaboksi ya kasi 4, pamoja na mipini ya kuingiza na kutoa nishati iliyolinganishwa, nguvu zake haziwezi kulinganishwa na nguvu za kiwango cha juu za uzungushaji za injini yoyote ya ndani ya Scania. Chaguo zinajumuisha Kidhibiti Mwendo cha Scania na aina mahususi za mifumo ya usambazaji wa nishati.
Gia za ekseli ya nyuma
Kampuni ya Scania inatoa aina mbalimbali za ekseli za kuendesha za mfumo mmoja wa kudhibiti kasi. Ekseli ya mfumo wa upunguzaji wa kasi pia inapatikana katika viwango viwilii. Ekseli ya R756 ambayo ni thabiti na nyepesi inatoa huduma bora na ya haraka ya kubadilisha gia, ambayo inaweka viwango vipya vya utendaji wa ekseli ya nyuma na kutoa utendaji ulioboreshwa wa mfumo wa uendeshaji wa Scania.
Ekseli ya kuendesha hebu yenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi
Ekseli za kuendesha hebu zenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi zinapatikana kwa ajili ya shughuli ambazo uwezo wa kuwashwa, nafasi kati ya fremu ya gari na barabara na kiwango cha juu zaidi cha uzito wa gari unaoruhusiwa vinafaa. Hudhibiti kiwango cha juu zaidi cha uzito wa gari kinachoruhusiwa cha hadi tani 80 na uwiano wa gia wa kuanzia 3.80 hadi 7.18.
Ekseli moja ya kuendesha yenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi
Gia zetu za kifaa kimoja cha kupunguza kasi zina kiwango cha chini cha mbano na utendaji wa kiwango cha juu na zinaweza kudhibiti kiwango cha juu zaidi cha uzito wa gari unaoruhusiwa wa hadi tani 78 na uwiano mkubwa wa gia kuanzia 1.95 hadi 5.57.
EKSELI MBILI ZA KUENDESHA ZENYE KIFAA KIMOJA CHA KUPUNGUZA KASI
Ekseli mbili za kuendesha zenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi zinatolewa kwa shughuli ambazo unahitaji kuvuta mizigo na matumizi ya kiwango cha chini cha mafuta. Gia ya kushuka ya RB662 + R660 hudhibiti kiwango cha juu zaidi cha uzito wa gari unaoruhusiwa wa hadi tani 80 na uwiano wa gia wa kuanzia 2.92 hadi 4.88.
Ekseli mbili za kuendesha hebu zenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi
Aina zetu nyingi za ekseli mbili za kuendesha hebu zenye kifaa kimoja cha kupunguza kasi ni thabiti na za kudumu na zinatoa huduma bora zaidi ya kuwashwa kwa injini na nafasi kubwa kati ya fremu ya gari na barabara. Hudhibiti kiwango cha juu sana cha uzito wa gari unaoruhusiwa wa hadi tani 210 na uwiano wa gia wa kuanzia 3.52 hadi 7.63.
UWIANO MPANA WA GIA
Ekseli ya R756 inatoa uwiano mpana wa gia kuanzia 1.95 hadi 4.11 na imebuniwa kudhibiti uzito mkubwa wa gari wa hadi tani 53 GTW.Info point 2 (+ on image)
WAKATI WA UTENDAKAZI USIO NA USHINDANI
The R756 is engineered to deliver extended oil change intervals and an increased component lifetime.
Mpangilio wa ekseli
Ekseli ya mbele, nyuma, isiyozunguka na inayozunguka – Scania inaweza kutimiza mahitaji ya shughuli yoyote. Msururu wa S unaweza kuunganishwa na anuwai ya mipangilio ya chesisi za Scania zenye urefu tofauti.
4x2
Kimo cha chesisi
Chini zaidi, chini, kawaida, juu
4x4
Kimo cha chesisi
High
6x2
Kimo cha chesisi
Kawaida
6x2/2
Kimo cha chesisi
Kawaida
6x2 ya kusukuma
6x2/4
Kimo cha chesisi
Kawaida, fupi
6x2 inaendeshwa na ekseli mbili
6x4
Kimo cha chesisi
Kawaida, refu
6x6
Kimo cha chesisi
High
4x2
Kimo cha chesisi
Chini, kawaida, juu
4x4
Kimo cha chesisi
High
6x2
Kimo cha chesisi
Fupi, kawaida
6x2/2
Kimo cha chesisi
Kawaida
6x2 ya kusukuma
6x2/4
Kimo cha chesisi
Kawaida
6x2 inaendeshwa na ekseli mbili
6x2*4
Kimo cha chesisi
Fupi, kawaida
6x4
Kimo cha chesisi
Kawaida, refu
6x6
Kimo cha chesisi
High
8x2
Kimo cha chesisi
Kawaida
8x2*6
Kimo cha chesisi
Fupi, kawaida
8x2 inaendeshwa na ekseli ya nyuma
8x2/4
Kimo cha chesisi
Kawaida
8x2 inaendeshwa na ekseli mbili
8x4
Kimo cha chesisi
Kawaida, refu
8x4*4
Kimo cha chesisi
Kawaida
8x4 inaendeshwa na ekseli ya nyuma
10x4*6
Kimo cha chesisi
Kawaida
10x4 inaendeshwa na ekseli ya nyuma
Wasiliana na muuzaji wako
Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.