Tanzania

Chesisi ya Scania K

Fremu fupi

Mitambo ya injini

Fremu fupi ya toleo la K ya Scania inatoa aina mbalimbali za mifumo ya uendeshaji ya kutegemewa na yenye matumizi bora ya nishati iliyoboreshwa kwa ajili ya magari ya usafiri wa ndani ya jiji na mitaani.

InjiniNguvu inayotolewaTokiUdhibiti wa uchafuziChaguzi za mafuta
Lita 9320 Hp (235kW)1600 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)Biodizeli, HVO, Dizeli
Mota ya umeme130 kW1030 NmHakuna uchafuziUmeme
Giaboksi:
Giaboksi ya kasi 12 na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania

UjazoNguvu inayotolewaTokiUdhibiti wa uchafuziChaguzi za mafuta
Lita 7280 Hp (206kW)1200 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)Biodizeli, HVO, Dizeli
Lita 9280 Hp (206kW)1400 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)HVO, Dizeli
Lita 9320 Hp (235 kW)1600 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)Biodizeli, HVO, Dizeli
Lita 9360 Hp (265 kW)1700 NmSelective Catalytic Reduction (SCR)Biodizeli, HVO, Dizeli
Lita 13370 Hp (272 kW)1900 NmSelective Catalytic Reduction (SCR) HVO, Dizeli
Ujazo wa mafuta:
Lita 140 hadi 360, lita 450 hadi 560 (imeunganishwa)
Giaboksi:
Giaboksi ya kasi 6 ya kiotomatiki kikamilifu
Giaboksi ya kasi 12 na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania

UjazoNguvu inayotolewaTokiUdhibiti wa uchafuziChaguzi za mafuta
Lita 9280 Hp (206 kW)1350 NmKurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR)Biogesi, Gesi asili
Lita 9340 Hp (250 kW)1600 NmKurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR)Biogesi, Gesi asili

Ujazo wa mafuta:

Lita 1260-1875
Giaboksi:

Giaboksi ya kasi 6 ya kiotomatiki kikamilifu
Giaboksi ya kasi 12 na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania

Ekseli

Fremu fupi ya toleo la K ya Scania inapatikana katika aina mbalimbali hali ambayo inaiwezesha kutimiza mahitaji mbalimbali ya matumizi.

 

4x2 - ekseli isiyodhibiti mzunguko wa magurudumu au ekseli inayodhibiti mzunguko wa magurudumu

6x2*4 - ekseli isiyodhibiti mzunguko wa magurudumu au ekseli inayodhibiti mzunguko wa magurudumu

6x2/2 - (iliyounganishwa) ekseli isiyodhibiti mzunguko wa magurudumu au ekseli inayodhibiti mzunguko wa magurudumu

Kiwango cha sakafu

Sehemu ya chini ya kuingilia na sakafu bapa hadi kwenye sehemu ya milango ya katikati inatoa uwezo sawa wa kufikiwa kama wa toleo la sakafu ya chini katika sehemu za katikati na mbele. Katika sehemu nyuma, sakafu iliyoinuka inakuwezesha kuona vizuri abiria. Njia pana ya katikati inachangia urahisi zaidi wa ufikiaji, starehe na kupanda na kushuka kwa abiria.

Vipengele vya muundo

Fremu fupi ya toleo la K ya Scania inatimiza mahitaji ya wateja katika kila bara. Kwa udhibiti kamili wa ubunifu na utengenzaji wa fremu na mfumo wa uendeshaji, kampuni ya Scania inatengeneza fremu za kutegemewa, za kudumu na za utendaji bora wa kipekee.

 

Fremu ya chesisi

Ekseli ya mbele yenye nguvu zaidi, pamoja na uwezo wa kutumia magurudumu mapana kwa sasa, inamaanisha kuwa uwezo wa kubeba mizigo umeongezeka kutoka tani 7.1 hadi 8.2. Hali hii inaruhusu kubeba abiria wengi zaidi. Hali hii pia inawezesha usambazaji bora wa uzito kati ya ekseli za mbele na nyuma, ambalo ni jambo la muhimu kwa magari ya umeme na yanayotumia mafuta. Pia, uzito wa fremu umepunguzwa kwa asilimia mbili (2%) (>100 kg) bila kuathiri uthabiti, hali ambayo inachangia matumizi ya mafuta ya kiwango cha chini.

Teknolojia ya nguvu za injini

Mifumo ya uendeshaji inaotegemewa zaidi, inayodumu na thabiti inawezesha hatua ya kuokoa mafuta kwa hadi 21%, hali ambayo inawezeshwa kupitia vigezo kadhaa kama vile; ubora wa injini (-6%), giaboksi iliyoboreshwa (-3%), kupunguzwa kwa uzito (-3%) na kuongezwa kwa kipengele cha kuwasha/kuzima (-6%).

Mfumo wa kuongeza na kupunguza joto

Mfumo wetu bora zaidi wa kuongeza na kupunguza joto unapunguza matumizi ya nishati, bila kujali hali ya anga. Mfumo wa kuongeza joto hurudisha nishati kwenye mfumo hatua ambayo husababisha mzunguko wa hewa unaokoa nishati na udhibiti wa hali ya kuongeza na kupunguza joto. Mfumo wa kupunguza joto pia umetengwa kutoka kwenye mfumo wa uendeshaji, hatua ambayo inasababisha kuwepo kwa mazingira ya starehe kila wakati.

Udhibiti wa muunganisho

Scania ina mfumo wa udhibiti unaoongoza katika sekta hii kwa vibadala vilivyounganishwa ambavyo vinatumia udhibiti wa kuzunguka kwa gurudumu, udhibiti wa kuvuta, mfumo wa kuondoa wa muunganisho na udhibiti wenye hati miliki. Hii huzuia kukosekana kwa uthabiti nakukunjika huku pia kuwezesha ushughulikiaji, udhibiti rahisi wakati wa uendeshaji, na uendeshaji salama katika hali ya utelezi na wakati wa mabadiliko ya njia katika mwendo wa kasi.

Eneo la dereva

Hutoa egonomiki bora kupitia marekebisho yote ya kiti cha kisicho na ngazi, paneli ya ala inayoweza kubadilishwa, uwekaji wa swichi unaonyumbulika . Paneli ya ala iliyo chini kiasi huongeza mwonekano. Mabasi hayo yana uwezo bora zaidi wa kuendesheka na yana eneo kubwa la kugeuza, mifumo ya hali ya juu ya usaidizi wa madereva, na ushughulikiaji ulioboreshwa wa kusaidiwa, usukani na breki. Pia, hutoa usalama ulioongezeka, mfumo bora wa hali ya hewa na mfumo mzuri wa kupunguza kelele na mitikisiko.

Teknolojia ya viangiko vya mbele

Bila kuathiri uwezo wa kubeba abiria, viangiko vipya vya mbele kwa kujitegemea hutoa starehe bora ya abiria na kuwezesha ujia mpana zaidi (900 mm) - na kusababisha uwezekano wa mpangilio mpya, kuongezeka kwa mtiririko wa abiria, nafasi na ufikiaji. Viangiko vipya imara vya mbele pia huongeza uwezo wa kubeba abiria na hutoa starehe nzuri ya abiria.

Endelea kuchunguza

Wasiliana na muuzaji wako

Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.

Pata tawi letu lililo karibu na wewe.
Call us
E-mail us
E-mail Workshop
View Dealer Website
OPENING HOURS
ACCEPTED CREDIT CARDS