Scania Irizar
i3LE & i4
Mitambo ya injini
Scania Irizar i3 ya muingilio wa chini na umbali mfupi wa unganisho wa miji Scania Irizar i4 inatoa aina mbalimbali za mitambo ya uendeshaji yenye ufanisi wa nguvu na za kutegemewa zilizoboreshwa kwa trafiki ya ndani ya jiji na vitongoji.
Injini | Nguvu inayotolewa | Toki | Udhibiti wa uchafuzi | Chaguzi za mafuta |
---|---|---|---|---|
Lita 9 | 320 Hp (235kW) | 1600 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Mota ya umeme | 130 kW | 1030 Nm | Hakuna uchafuzi | Umeme |
Giaboksi: Giaboksi ya kasi 12 na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania |
Ujazo | Nguvu inayotolewa | Toki | Udhibiti wa uchafuzi | Chaguzi za mafuta |
---|---|---|---|---|
Lita 7 | 280 Hp (206kW) | 1200 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Lita 9 | 280 Hp (206kW) | 1400 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | HVO, Dizeli |
Lita 9 | 320 Hp (235 kW) | 1600 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Lita 9 | 360 Hp (265 kW) | 1700 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Lita 13 | 370 Hp (272 kW) | 1900 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | HVO, Dizeli |
Ujazo wa mafuta: Lita 140 hadi 360 Giaboksi: Giaboksi ya kasi 6 ya kiotomatiki kikamilifu Giaboksi ya kasi 12 na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania |
Ujazo | Nguvu inayotolewa | Toki | Udhibiti wa uchafuzi | Chaguzi za mafuta |
---|---|---|---|---|
Lita 9 | 280 Hp (206 kW) | 1350 Nm | Kurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR) | Biogesi, Gesi asili |
Lita 9 | 340 Hp (250 kW) | 1600 Nm | Kurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR) | Biogesi, Gesi asili |
Ujazo wa mafuta: Lita 1260-1875 Giaboksi ya kasi 6 ya kiotomatiki kikamilifu |
Ujazo | Nguvu inayotolewa | Toki | Udhibiti wa uchafuzi | Chaguzi za mafuta |
---|---|---|---|---|
Lita 9 | 280 Hp (206kW) | 1400 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Lita 9 | 320 Hp (235 kW) | 1550 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Lita 9 | 360 Hp (265 kW) | 1700 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Ujazo | Nguvu inayotolewa | Toki | Chaguzi za mafuta |
---|---|---|---|
Lita 9 | 250 Hp (184 kW) | 1250 Nm | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Lita 9 | 310 Hp (228 kW) | 1550 Nm | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Ekseli, milango, urefu
Masafa ya Scania Irizar ya mijini yanapatikana katika matoleo tofauti na chaguzi kadhaa za usanidi wa milango ili kuweza kukidhi mahitaji tofauti ya uwezo wa kubeba abiria na mtiririko wa abiria.
Juu
Urefu unaweza kutofautiana kulingana na soko, mitambo ya nguvu ya uendeshaji na usanidi.
i3: 3.399 m
i4: 3.405 m
Vipengele vya muundo
Mabasi yetu yanazalishwa kwa ushirikiano wa muda mrefu kati ya Scania na Irizar. Kila kitu kutoka kwa ujenzi wa chesisi hadi mitambo ya nguvu ya uendeshaji na mwili imetengenezwa na kujaribiwa kikamilifu kwa kuzingatia kutegemeka na utendakazi bila kuathiri ufanisi wa nguvu.
Fremu ya chesisi
Ekseli ya mbele iliyoimarishwa inamaanisha kuwa uwezo wa mzigo umeongezeka kutoka tani 7.5 hadi 8.2. Hii inaruhusu uwezo wa juu wa kubeba mzigo. Pia huwezesha usambazaji wa uzito ulioboreshwa kati ya ekseli za mbele na za nyuma, ambayo ni muhimu sana kwa magari ya umeme na gesi.
Teknolojia ya nguvu za injini
Mifumo ya uendeshaji inaotegemewa zaidi, inayodumu na thabiti inawezesha hatua ya kuokoa mafuta kwa hadi 21%, hali ambayo inawezeshwa kupitia vigezo kadhaa kama vile; ubora wa injini (-6%), giaboksi iliyoboreshwa (-3%), kupunguzwa kwa uzito (-3%) na kuongezwa kwa kipengele cha kuwasha/kuzima (-6%).
Teknolojia ya viangiko vya mbele
Bila kuathiri uwezo wa kubeba abiria, viangiko vipya kwa mbele vya kujitegemea vinatoa starehe bora. Viangiko vipya vya mbele imara pia huongeza uwezo wa kubeba abiria na hutoa starehe nzuri pamoja na njia pana na ya chini ya basi ya sitahani mbili.
Mfumo ya umeme
Usanifu mpya wa usambazaji wa nishati unakuja na vitengo vilivyoboreshwa vya udhibiti wa kielektroniki (ECUs) na utendaji ambao huboresha utendakazi na kuwezesha uchunguzi kwa ukarabati na matengenezo. Pia huwezesha utendakazi mpya ndani ya ADAS, uhamaji wa kielektroniki na mifumo ya usafiri unaojiendesha.
Vipengele vya usalama
Mabasi ya Scania yana mifumo ya hali ya juu ya usaidizi wa madereva (ADAS) ikijumuisha onyo la kugongana kwa watumiaji wa barabara walio hatarini, onyo la mahali pasipoonekana, udhibiti wa kasi ya usafiri unaobadilika, usaidizi wa tahadhari, na breki za dharura za hali ya juu. Zaidi ya hayo, teknolojia ya breki ya maegesho ya nyumatiki huepuka mwendo wa basi bila kukusudia na hivyo basi ajali zinazoweza kutokea. Kupitia ujenzi wa miili iliyoimarishwa na chesisi, mabasi yetu yanajengwa kulinda abiria, madereva na vifaa nyeti.
Ubunifu wa mambo ya ndani
Starehe bora ya abiria na viti vya egonomiki, kupunguza uzalishaji wa kelele na mitetemo. Kusafisha kila siku ni rahisi kwa vifaa na teknolojia za kisasa za utengenezaji kuboresha uimara, kuzeeka, na kutumika tena.
Endelea kuchunguza
-
-
Scania Citywide LE
Scania Citywide yenye muingilio wa chini limeundwa na kutayarishwa na Scania. Kila kitu kutoka kwa ujenzi wa chasi hadi mwili kimetengenezwa na kupimwa kabisa kwa kuzingatia kuegemea na utendaji. -
Fremu ya LE ya toleo la K ya Scania
Fremu fupi ya toleo la K ya Scania inatimiza mahitaji ya wateja katika kila bara. Kwa udhibiti kamili wa ubunifu na utengenzaji wa fremu na mfumo wa uendeshaji, kampuni ya Scania inatengeneza fremu za kutegemewa, za kudumu na za utendaji bora wa kipekee. -
Scania Interlink
Basi la Scania Interlink limetengenezwa kwa njia mahiri. Ni basi letu linaloweza kubadilika zaidi. Unaweza kuamua idadi kamili ya wasafiri, mpangilio wa viti na milango. Lina nafasi nzuri ya ndani na nafasi ya kusimama au kutembea. Rafu za kupendeza za kuweka mizigo, paneli za taa, matakia na mengine mengi. -
Chesisi ya Scania K HF Urban
Chesisi ya Scania K yenye sakafu ya juu inakidhi mahitaji ya waendeshaji katika kila bara. Kwa muundo kamili na udhibiti wa uzalishaji juu ya chesisi na mitambo ya nguvu, Scania hutoa utegemeo usio na mpinzani, uimara na utendakazi usio na kifani. -
Scania Fencer
Scania Fencer imeundwa na kuzalishwa kwa ushirikiano kati ya Scania na Higer. Kila kitu kutoka kwa ujenzi wa chesisi hadi mitambo ya nguvu ya uendeshaji na mwili imetengenezwa na kujaribiwa kikamilifu kwa kuzingatia kutegemeka na utendakazi bila kuathiri ufanisi wa nguvu. Mchakato wa kawaida wa kujenga mwili wa Fencer wa Scania hupunguza wakati wa uzalishaji na hutoa huduma ya hali ya juu kupitia ujanibishaji wa vipuri. -
Scania Irizar
Mabasi yetu yanazalishwa kwa ushirikiano wa muda mrefu kati ya Scania na Irizar. Kila kitu kutoka kwa ujenzi wa chesisi hadi mitambo ya nguvu ya uendeshaji na mwili imetengenezwa na kujaribiwa kikamilifu kwa kuzingatia kutegemeka na utendakazi bila kuathiri ufanisi wa nguvu.
Wasiliana na muuzaji wako
Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.