Scania Interlink
Sitaha fupi
Mifumo ya uendeshaji
Basi la Scania Interlink lenye sitaha fupi lina aina mbalimbali za mifumo ya uendeshaji ya kutegemewa na yenye matumizi bora ya nishati iliyoboreshwa kwa ajili ya usafiri wa mitaani na eneo.
Mfumo wa uendeshaji | Kiwango cha usambazaji wa nishati | Nguvu ya kuzungusha | Udhibiti wa utoaji gesi ya kaboni | Chaguo za mafuta |
---|---|---|---|---|
Injini ya lita 9 ya mafuta | 320 hp (235kW) | 1600 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, dizeli |
Mota ya kielektroniki | 130 kW | 1030 Nm | ||
Kiwango cha mafuta:
|
Kiwango | Kiwango cha usambazaji wa nishati | Nguvu ya kuzungusha | Udhibiti wa utoaji gesi ya kaboni | Chaguo za mafuta |
---|---|---|---|---|
Lita 9 | 280 hp (206 kW) | 1350 Nm | Kurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR) | Biogesi, gesi asili |
Lita 9 | 340 hp (250 kW) | 1600 Nm | Kurudi tena kwa gesi ya ekzosi kwenye injini (EGR) | Biogesi, gesi asili |
Kiwango cha mafuta: Lita 700 (LBG/LNG) Giaboksi: Giaboksi ya kasi 6 ya kiotomatiki (ZF EcoLife 2) Giaboksi ya kasi 12 isiyo ya kiotomatiki na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania na kipunguza mwendo |
Kiwango | Kiwango cha usambazaji wa nishati | Nguvu ya kuzungusha | Udhibiti wa utoaji gesi ya kaboni | Chaguo za mafuta |
---|---|---|---|---|
Lita 7 | 280 hp (206kW) | 1200 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, dizeli |
Lita 9 | 280 hp (206kW) | 1400 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, dizeli |
Lita 9 | 320 hp (235 kW) | 1600 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, dizeli |
Lita 9 | 360 hp (265 kW) | 1700 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, dizeli |
Kiwango cha mafuta: Giaboksi: Giaboksi ya kasi 12 isiyo ya kiotomatiki na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania na kipunguza mwendo |
Ekseli, milango, urefu
Basi la Scania Interlink lenye sitaha fupi linapatikana katika aina mbalimbali, hali ambayo inaliwezesha kutimiza mahitaji mbalimbali ya matumizi.
Urefu
Urefu wa basi la Scania Interlink unategemea chaguo la uendeshaji na matangi ya gesi na vijenzi vya kielektroniki vilivyowekwa kwenye paa.
Mita 3.31 (dizeli, biodizeli, LBG/LNG)
Mita 3.53 (muundo mseto)
Mita 3.64 (CBG/CNG)
Kiwango cha sakafu
Basi linaweza kupandwa kwa urahisi na wasafiri wote na sakafu isiyo na stepu kwenye njia yote iliyo baina ya viti. Ambalo linaweza kupandwa kwa stepu chache unapopanda gari. Kuna pia uwezekano wa kuweka lifti ya kiti cha magurudumu kwenye milango ya katikati.
Sakafu iliyoinuka inaboresha starehe ya wasafiri, mwonekano na chaguo la nafasi ya kuweka mizigo.
Vipengele vya muundo
Basi la Scania Interlink lenye sitaha fupi linatimiza mahitaji ya waendeshaji. Kwa udhibiti kamili wa ubunifu na utengenzaji wa fremu na mfumo wa uendeshaji, basi la Scania linatoa huduma ya kutegemewa, ya kudumu na utendaji bora wa kipekee.
Uwezo wa kurekebishwa kwa vipimo
Basi la Scania Interlink lina uwezo mkubwa wa kurekebishwa kuhusiana na kufupishwa kwa urefu wa gari kulingana na urefu mahususi, mpangilio wa ndani, uainishaji na mengineyo.
Pia, muundo mseto na aina nyingi za chaguo za mafuta yanayoweza kutumika tena zinaweza kupunguza utoaji wa gesi ya CO2 kwa hadi kiwango cha 90 %.
Vipengele vya usalama
Mabasi ya Scania yana mifumo ya kina ya usaidizi wa dereva (ADAS) ikijumuisha onyo la uwezekano wa kugongana na mtumiaji mwingine wa barabara, onyo la sehemu isiyoonekana vizuri, udhibiti wa kasi unaoweza kubadilika, usaidizi wa kumakinika na breki za kina za dharura. Kando na hayo, teknolojia ya mfumo wa udhibiti wa breki za kuegesha zinazotumia shinikizo la hewa huzuia basi kusonga bila kutarajiwa na hivyo basi kuepuka ajali zinazoweza kutokea. Kupitia utengenezaji wa fremu na umbo thabiti, mabasi yetu yametengenezwa ili kulinda usalama wa wasafiri, madereva na vijenzi nyeti. Pamoja na Scania Zone – ambayo huhakikisha kufuata udhibiti wa kasi – hatua hizi zote husaidia kuepuka ajali. Na muda wa matengenezo.
Sehemu ya dereva
Inakupa hali na ufanisi wa uendeshaji kupitia urekebishaji wa kiti katika pembe zote bila kufuata hatua zozote, paneli ya vifaa inayoweza kurekebishwa, uwekaji wa swichi inayoweza kubadilishwa n.k. Paneli fupi ya vifaa, nguzo nyembamba za A- na B-, dirisha la chini la kando na dirisha kubwa la mbele na vipengele vingine huongeza uwezo wa kuona. Mabasi haya yana uwezo bora zaidi wa kuendeshwa na nafasi bora ya kiwango cha chini zaidi ya kugeuka, mifumo ya kina ya usaidizi wa dereva na mifumo iliyoboreshwa ya ushughulikiaji, uendeshaji na kushika breki. Pia, yana usalama ulioboreshwa, mfumo bora wa kurekebisha halijoto na uwezo mzuri wa kupunguza kelele na mitetemo.
Fremu na mfumo wa uendeshaji
Kwa ufansi ulioboreshwa wa injini na giaboksi, huokoa mafuta kwa hadi kiwango cha 8 %, huku vipengele vya kuwasha/kuzima na udhibiti wa kasi vikichangia zaidi katika upunguzaji wa gharama na utoaji wa gesi.
Maboresho mengine ya fremu yanajumuisha kuongeza kilo 500 za uwezo wa kubeba mizigo kwenye ekseli ya mbele na sehemu huru ya mbele ambayo inaboresha starehe ya uendeshaji.
Muundo wa ndani
Muundo mpya wa sehemu ya ndani unatengeneza mazingira ya kupendeza zaidi kwa wasafiri, hali ambayo inaongeza mvuto wa usafiri wa umma. Rangi za angavu kwenye dari na paneli za kando na rafu za wazi za kuweka mizigo zinatengeneza mazingira angavu na ya kupendeza. Pamoja na vijenzi vya kupunguza sauti vinavyochangia kutengeneza mazingira tulivu na ya kupendeza kwa dereva na wasafiri.
Muundo wa nje
Muundo wa nje wa kisasa na changamano wa basi la Scania Interlink unaashiria ubunifu, ubora na mawazo endelevu. Lina umbo dogo, mtindo wa kimtindo kwenye pande zake na madirisha hadi kwenye kifuniko cha buti. Ikijumuishwa na ulinzi wa paa kwa ajili ya vijenzi kama vile sehemu za AC, matangi ya gesi na vifurushi vya betri. Chaguo mpya za taa za mbele kwa ajili ya kuona vizuri na chaguo la kuwa na taa za ziada za LED na taa za kupiga kona kwa ajili ya kuboreshwa kwa hali ya kuona ya dereva.
Endelea kugundua
-
-
-
-
Fremu ya LE ya toleo la K ya Scania
03 Feb 2022 Fremu fupi ya toleo la K ya Scania inatimiza mahitaji ya wateja katika kila bara. Kwa udhibiti kamili wa ubunifu na utengenzaji wa fremu na mfumo wa uendeshaji, kampuni ya Scania inatengeneza fremu za kutegemewa, za kudumu na za utendaji bora wa kipekee. -
Wasiliana na muuzaji wako
Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.