You seem to be located in .

Go to your Scania market site for more information.

Utengenezaji wa magari ya kielektroniki

Siku za usoni, kila mfumo wa usafiri unaweza kuwa wa kielektroniki. Na ili kuunda ulimwenguni bora zaidi, mifumo mingi ya usafiri italazimika kuwa ya kielektroniki. Aina nyingi za malori, mabasi na injini za kielektroniki za kampuni ya Scania zinapatikana hapa na sasa, ambazo ziko tayari kupunguza utoaji wa gesi ya kaboni kutokana na shughuli zako.

Kila mwaka, kampuni ya Scania itazindua angalau bidhaa moja mpya ya kielektroniki, ili kushughulikia mahitaji yote ya usafiri, ikijumuisha usafiri wa masafa marefu.

Teknolojia ya betri

Kadri teknolojia ya utengenezaji wa magari ya kielektroniki inavyozidi kukua kwa haraka, hatua ya kuendelea kuboresha betri inahitajika ili kutengeneza betri zinazofaa kwa mahitaji usafiri mzito wa wateja wetu.

 

Kampuni ya Scania imeshirikiana na kampuni ya Northvolt katika mchakato wa kampuni hii ya Kiswidi wa utengenezaji wa betri. Kampuni ya Scania inapanga pia kuwekeza zaidi ya kiasi cha SEK bilioni 1 kwenye kampuni ya ukusanyaji wa vipuri vya betri katika jiji la Södertälje, Uswidi. Kampuni hii inayochukua nafasi ya mita mraba 18,000 itaanza kufanya kazi kikamilifu kufikia mwaka wa 2023, ambapo itakusanya vifurushi vya vipuri vinavyofaa kwa utengenezaji wa betri za bidhaa za kampuni ya Scania.

 

Vile vile, kampuni ya Scania inajenga pia maabara mpya ya betri katika mijengo yake ya utafiti na utengenezaji katika jiji la Södertälje. Maabara haya yataanza kutumika kikamilifu mwishoni mwa mwaka wa 2021 na yana kumbi tatu za majaribio ya betri, moduli na vifurushi. 

Teknolojia ya betri ya nishati ya umeme ya haidrojeni

Malori ambayo yanatumia mfumo wa kielektroniki kikamilifu, yana mfumo wa uendeshaji wa kielektroniki na nishati hubadilishwa kuwa umeme kutoka kwenye gesi ya haidrojeni katika betri za nishati ya umeme zilizowekwa kwenye magari hayo. Malori yanayotumia nishati ya betri ya umeme yana pia betri ya kawaida ili kutumiwa wakati ambapo nishati ya ziada inahitajika na wakati ambapo gari linahitaji kuchaji tena nishati ya umeme kutoka kwenye nguvu za breki.

Teknolojia hii inavutia wakati ambapo magari yanayotumia nishati ya betri yamekumbwa na hitilafu ya kiufundi au ya kiutendakazi kama vile uzito wa shehena, masafa au nafasi ya fremu.

 

Mapungufu ya teknolojia hii ni kiwango chake cha jumla cha nishati ambacho ni cha chini kuliko BEV, pamoja na swali muhimu kuhusu mahali na jinsi ya kutengeneza gesi ya haidrojeni. Kigezo muhimu zaidi cha mustakabali wa teknolojia hii ni upatikanaji na bei ya gesi ya haidrojeni inayoweza kutumika tena siku za usoni.

Wasiliana na muuzaji wako

Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.

Ikiwa na chaguo nyingi mno na mpangilio wa mipangilio ya wastani, unaweza kuweka mipangilio inayokufaa kwenye lori lako. Ifanye iwe Scania.