Lori linalotumia nishati ya betri
Ungependa tuwasiliane nawe ili tufanye mkutano wa kibinafsi au kuwasiliana na mtaalamu wa masuala ya kubadilisha teknolojia za kutumia mafuta na kuanza kutumia teknolojia za umeme kama chanzo cha nishati?
MABADILIKO YA KUACHA KUTUMIA TEKNOLOJIA ZA KUTUMIA MAFUTA NA KUANZA KUTUMIA TEKNOLOJIA ZA KUTUMIA UMEME KAMA CHANZO CHA NISHATI YANABADILISHA KILA KITU – ISIPOKUWA AHADI YETU
Umeweza kutegemea kampuni ya Scania kila wakati kwa kupata suluhu kamili kwa kazi yako – na hilo halitabadilika. Hata hivyo, mabadiliko ya kuacha kutumia teknolojia za kutumia mafuta na kuanza kutumia teknolojia za kutumia umeme yanaleta changamoto mpya ambazo zinaweza kuonekana kuwa ngumu.
Ahadi yetu: Huhitaji kuwazia suala hili peke yako
Tutakuwa nawe kwa kila hatua, na kuhakikisha unapata kifaa kinachotumia umeme ambacho si bora tu kwa mazingira, lakini pia kinachofaa kwa kazi yako.
Kifaa chetu ndicho suluhisho
Kutoka katika kampuni ya Scania, hutapata tu lori la kawaida na kuachwa ukiwa na maswali au wasiwasi. Kwa magari yetu ya umeme, pindi unapopokea funguo za malori yako – tunahakikisha kuwa yanaweza:
- Kuchajiwa, kuendeshwa, kufanyiwa matengenezo, kukarabatiwa, kurekebishwa, kufadhiliwa na kupewa bima – ipasavyo
Lakini pia unapata:
- Ushauri wa kudumu na wa mara kwa mara na maelekezo kutoka kwa wataalamu wetu wa magari ya teknolojia ya umeme
Gari hili ni kifurushi kilicho na kila kitu, lililobuniwa ili kufaa kwa kazi yako – na lililoundwa kwa kuzingatia msingi wa kutengeneza magari bora ya umeme.
Lori linalotumia nishati ya betri la Scania
Vipimo vya BEV
MPANGILIO WA MAGURUDUMU
4x2, 6x2, 6x2*4
UMBALI WA EKSELI
3950 – 5750 mm
CHAGUZI ZA KEBINI
P, L
UENDESHAJI
Mashine ya umeme ya sumaku ya kudumu yenye kupozea mafuta.
~295 kW 2,200 Nm (Kilele)
~230 kW 1,300 Nm (ya kuendelea)
60 kW Nguvu ya Umeme ya Kuondoa
UWEZO WA BETRI
Betri 9 za Ioni za Lithi, zinapatikana kwa umbali wote wa ekseli zaidi ya 4350mm:
300 kWh (Imesakinishwa)
Betri 5 za Ioni za Lithi, zinapatikana kwa umbali wote wa ekseli zaidi ya 3950 mm:
165 kWh (Imesakinishwa)
KUCHAJI
Muunganisho wa programu-jalizi ya aina 2 ya CCS hadi 130 kW / 200A DC kuchaji
GTW
Upeo 29 t
Ufafanuzi wa magari ya Scania
Mfumo wa kuchaji na muundo msingi
Ili kutumia magari ya umeme, unatakiwa kufikiria zaidi kuliko tu kufikiria kuhusu mahali pa kuyachaji na wakati wa kuchaji. Tunachanganua kazi yako na kukusaidia kuweka mpango wa kupata suluhu kamili, na muunganisho wa gridi, maunzi ya mfumo wa kuchaji na hata mikataba ya nishati safi.
Matengenezo kwa ajili ya matumizi ya muda mrefu
Magari ya umeme yana faida ya kutokuwa na sehemu nyingi za kuendeshwa – hali ambayo kwa jumla inapunguza mahitaji ya kufanya matengenezo. Lakini mahitaji ambayo bado yapo ni mapya na tofauti, kuhitaji leseni za matumizi ya volteji ya kiwango cha juu na zana maalum. Karakana zetu zina uwezo wa kushughulikia haya yote.
Mchakato wa mauzo ya mashauriano na huduma zinazofaa
Huduma, ushauri na usaidizi mahususi wa kitaalamu ambao biashara yako inahitaji unaweza kutofautiana na biashara nyingine. Tunakupa kifurushi kinachofaa kwa kazi yako, kulingana na uchanganuzi wa kina – ili kuhakikisha kuwa kazi yako inafanyika kwa njia bora na kwamba unahisi kupokea usaidizi wa muda mfupi na wa kudumu.
Masafa na nishati
Mfumo wa uendeshaji unaotumia umeme unatoa nishati ya kiwango cha kutosha na nguvu za kuzungusha mfumo papo hapo. Kuwasha kwa kutumia mfumo kamili wa umeme huwezesha vitengo vyote viwili vya haidroli na friji kuendelea kufanya kazi bila kutoa gesi yoyote ya kaboni. Kwa kwenda hadi umbali wa kilomita 250 kwa kuchaji mara moja, unaweza kusafiri masafa mafupi na ya kati kwa kutumia nishati kamili ya umeme.
Zaidi ya shughuli za usafiri
Uwezo wa kutekeleza shughuli za usafiri bila utoaji wa gesi yoyote ya kaboni ni masharti ya kawaida yanayozidi kuzingatiwa ili kupata mikataba mipya, bila kujali iwapo unafanya kazi ya usambazaji wa bidhaa – au unafanya kazi ya kukusanya taka, lifti za kunyanyua mizigo, malori ya kumwaga mchanga au mashine za kuchanganya zege. Kwa hivyo, si tu suala la uwekezaji katika kundi lako la magari, lakini pia katika kampuni yako, ushindani wa soko na mustakabali wako.
Inadumu kweli
Sisi huweka mpango wa kudumu ili kuhakikisha betri zetu zinaweza kutumiwa kwa madhumuni mengine au kutumika upya baadaye. Tukiwa na washirika wetu katika sekta ya nishati na muundo msingi, tunaweza kukupatia anwani hizo ili kukusaidia uanzishe ushirikiano si tu kwa ajili ya kupata vifaa vya mfumo wa kuchaji vinavyofaa kabisa kwa kazi yako – lakini pia na mikataba ya nishati safi ya umeme inayoweza kutumika tena.
KIFAA KILICHOTAYARI KUTUMIKA
Shughuli za biashara za kutumia umeme ni changamano zaidi. Kwa sababu hiyo, kila gari la umeme linalouzwa linatolewa kama kifaa kilichotayari kutumika, huduma za bima, ushauri na maelekezo ya kudumu, pamoja na vipengele vya mfumo wa kuchaji na mkataba wa nishati. Limeundwa ili kufaa kikamilifu kwa mahitaji na masharti yako kwa njia halisi – na kutofautiana katika aina ipasavyo.
UNGEPENDA KUFANYA MAWASILIANO YA SIMU AU MKUTANO WA BINAFSI?
Ungependa kupata maelezo zaidi kuhusu vifaa vyetu vya umeme tunavyotoa, au una maswali maalum? Weka maelezo yako ya mawasiliano hapa, na tutawasiliana nawe ili kupanga mawasiliano ya simu au mkutano ili kujadiliana kuhusu mahitaji na mipango yako ya kubadilisha teknolojia za kutumia mafuta na kuanza kutumia teknolojia za kutumia umeme kama chanzo cha nishati katika kazi yako.