You seem to be located in .

Go to your Scania market site for more information.

Kampuni ya Scania yaongeza kiwango chake cha uwekezaji katika kampuni ya Northvolt

Mwaka wa 2018, kampuni ya Scania ilitangaza kuwekeza katika Northvolt na ushirikiano wa kutengeneza na kuuza teknolojia ya betri ya magari yote ya kufanya kazi nzito. Kampuni hizi pia zimeweka makubaliano kuhusu kiwango cha kujitolea na uwezo wa betri wa siku za usoni. Kampuni ya Northvolt inapokamilisha sasa utoaji mwingine wa hisa, kampuni ya Scania inatangaza ongezeko sawa la kiwango cha uwekezaji wake katika ushirikiano huo.

Teknolojia ya utengenezaji wa magari ya umeme inazidi kuboreshwa kwa kasi. Kwa mabasi na malori makubwa, kuendelea kuboreshwa kwa mfumo wa kuchaji na betri kunahitajika. Kasi ya mabadiliko katika sekta ya utengenezaji wa betri ni ya juu huku hatua kubwa zikiwa zimepigwa katika miaka michache iliyopita ili kutengeneza betri zinazofaa kwa magari makubwa. Ushirikiano na kampuni ya Northvolt ni mojawapo ya miradi kadhaa ya kimkakati katika lengo la kampuni ya Scania la kuendeleza mabadiliko ya kutengeneza bidhaa za kudumu za usafiri.

 

"Kampuni ya Scania imekuwa mshirika muhimu wa kampuni ya Northvolt kuanzia mwanzoni. Tunatarajia kuendelea kuimarisha ushirikiano huu kwa miaka ijayo tunapoongeza kiwango chetu cha utengenezaji wa betri ili kuendeleza malori mapya ya kielektroniki ya Scania, anasema " Peter Carlsson, Mwanzilishi Mwenza na Afisa Mkuu Mtendaji wa kampuni ya Northvolt.

 

Kwa hatua yake ya hivi karibuni zaidi ya kutoa hisa, kampuni ya Northvolt inapanga kuwekeza katika upanuzi wa uwezo wa utengenezaji pamoja na R&D na shughuli za kutumia tena bidhaa zilizotumika, ili kuendeleza lengo la kuanzisha uwezo wa utengenezaji wa bidhaa wa kiwango cha 150 GWh katika bara la Ulaya kufikia mwaka wa 2030. Hili ni lengo muhimu hasa kwa kampuni ya Scania. Tayari betri zinahitajika kwa kiwango cha juu na mahitaji yake yanaendelea kuongezeka. Hata hivyo, kufikia sasa, kuna usambazaji mdogo wa betri na usambazaji mdogo hata zaidi wa betri zilizotengenezwa kwa ubora wa juu.

 

“Kwa sasa, ununuzi na utengenezaji wa betri kwa njia ya kudumu ni changamoto katika sekta nzima ya magari. Kampuni ya Northvolt ilianzishwa kwa dhamira ya kuunda betri ya nishati inayoweza kutumika tena duniani kote, inayotoa kiwango kidogo zaidi cha kaboni na uwezo wa kiwango cha juu wa kutumika tena. Hiyo ndiyo maana tunafikiria kuwa dhamira ya kampuni ya Northvolt inalingana zaidi na lengo na kusudi la kampuni ya Scania la kuleta mabadiliko ya mfumo thabiti wa usafiri”, anasema, Anders Williamsson, Mkuu wa Masuala ya Ununuzi katika kampuni ya Scania.