Moto na uokoaji
Tunakusaidia ubadilishe upendavyo malori yako ya Scania ya shughuli za zimamoto na uokoaji ili kuboresha uwezo na kurahisisha kazi yako.
Yameundwa kwa ajili ya shughuli za dharura
Kama vile wateja wetu wazimamoto, hatupuuzi chochote. Hakuna chochote ambacho hakijashughulikiwa katika utengenezaji wa magari haya mapya ya zimamoto. Matokeo yake ni aina magari thabiti na ya kutegemea zaidi.
Gundua malori ya shughuli za zimamoto na uokoaji
Gari la zimamoto
Gari la zimamoto ni kifaa cha kwanza cha mashambulizi na madhumuni ya msingi ni pamoja na kusafirisha wazimamoto hadi eneo la tukio, kutoa maji na kubeba vifaa vingine vinavyohitajika.
Magari ya kubeba maji/povu
Gari la kubeba maji/povu ni muundo maalum wa vifaa vya kuzima moto ili kusafirisha maji hadi kwenye eneo la moto. Kwa kawaida inasaidia vifaa vya mstari wa mbele au hufanya kazi katika mitambo ya mafuta, kemikali au umeme.
Ngazi zinazogeuzwa na majukwaa ya Angani
Vikosi vingi vya zimamoto vinahitaji kuwa na ngazi ya kugeuka kwenye magari yao au jukwaa la anga na urefu wa kufanya kazi hadi mita 40, wakati mwingine hadi mita 100.
Yenye matumizi mengi
Katika baadhi ya matukio kuna haja ya gari kuwa rahisi kubadilika; kuondoka kwenye eneo la tukio na kurudi ndani ya dakika chache kama gari la kubeba maji/povu au hata ambulensi iliyo na vifaa kamili. Huo ni ubadilikaji wa lifti ya ndoana.
Magari ya moto ya viwandani
Magari ya moto ya viwandani yana matumizi maalum sana, yanayotumika katika viwanda vya kusafisha mafuta au viwanda vya kemikali za petroli.
Usalama
Huduma za dharura na vikosi vya zimamoto vinahitaji kubeba wafanyakazi na vifaa haraka na kwa usalama. Usalama na ustawi wa wanatimu ulikuwa kipengele cha msingi katika utengenezaji wa magari mapya ya Scania CrewCab. Wafanyakazi wote wanaweza kulindwa na mifuko minne ya hewa ya pazia la upande.
Wakati wa kufanyakazi
Kuwa na gari la kuaminika wakati wa kutekeleza huduma za dharura ni muhimu. Malori ya zimamoto na uokoaji ya Scania ni matokeo ya miaka mingi ya utengenezaji wa malori ya ubora wa juu na ushirikiano wa karibu na wajenzi mahususi wa miili. Hii, pamoja na mipango yetu ya matengenezo inayoweza kubadilika ambayo huhakikisha kwamba kila lori moja linapata matengenezo yanayofaa kwa wakati unaofaa hasa, unapunguza muda wako wa kupumzika usiotarajiwa.
Tija
Katika Scania, tunaangazia biashara yako. Yote ni juu ya kuboresha tija, kuongeza urahisi wa ufikiaji na kupunguza muda unaohitajika ili kutekeleza shughuli husika.
Suluhu za huduma
Kampuni ya Scania husaidia kuhakikisha utendaji wako kwa kutoa huduma nyingi zilizobuniwa ili kufaa kwa kazi zako mahususi. Kitu chochote ambacho kinaweza kuboresha faida yako, utapata suluhu ya huduma ya Scania inayoishughulikia, kuanzia kwa ufadhili na kupata mafunzo ya udereva na huduma za ukarabati.
Mafunzo ya udereva
Wakufunzi wetu wa madereva walioidhinishwa hutumia mbinu mpya zaidi za ukufunzi na mafunzo ya udereva.
Ukarabati na matengenezo
Tunapanga mipango ya urekebishaji inayolingana na biashara yako, kuhakikisha muda wa kufanya kazi zaidi, kuongeza tija na kupunguza usumbufu katika utendakazi wako wa kila siku.
Gundua miundo ya malori ya Scania inayopendekezwa kwa shughuli za uchukuzi za zimamoto na uokoaji
Wasiliana nasi
Wasiliana nasi kwa njia inayokufaa, tafadhali teua chaguo lako hapa chini:
Badilisha upendavyo lori lako kwa uwezo bora
Tumia zana yetu ya usanidi iliyo rahisi kutumia ili ubadilishe upendavyo lori lako ili kuboresha tija na ufanisi. Jenga lori lako bora! Libadilishe liwe Scania.
Tafuta muuzaji aliyekaribu nawe
Wasiliana na wauzaji wetu walioidhinishwa ukiwa na maswali yoyote kuhusu bidhaa, huduma, au shughuli zetu katika eneo lako. Wasiliana nasi leo kwa msaada na usaidizi wa kitaalamu.