Usafiri katika uwanja wa ndege
Tunakusaidia ubadilishe upendavyo malori yako ya Scania kwa shughuli za usafiri katika uwanja wa ndege ili kuongeza uwezo na kurahisisha kazi yako.
Kwa wakati unaofaa - sharti la ratiba ngumu
Ingawa siku zako za kukaa katika uwanja wa ndege zinaweza kutofautiana, kuna hali za utofauti ambazo zinafanana. Hitaji la kutunza mazingira na urahisi wa kubadilika pamoja na ratiba yenye shughuli nyingi. Kwa bahati nzuri, urahisi wa kubadilisha shughuli zetu ni kitu tunachothamini katika kampuni ya Scania. Kwa kutumia mfumo wetu unaoweza kubadilika kama rasilimali yetu kuu zaidi, tunaweza kutengeneza bidhaa za kufaa karibu kazi yoyote. Ikiwa ni pamoja na yako.
Kufagia barabara ya ndege
Kwa kutegemea ukubwa na wingi wa shughuli, uwanja wa ndege unaweza kuwekewa fagio kubwa mahususi za kufagia barabara ya ndege na fagio ndogo zaidi za kufagia maeneo ya teksi na huduma.
Huduma ya uchukuzi wa chakula katika uwanja wa ndege
Malori ya uchukuzi wa chakula yanapatikana katika ukubwa tofauti na yanaweza kuwekewa vyumba vidogo vyenye halijoto zinazodhibitiwa. Ufanisi huzidishwa ikiwa lori linaweza kubeba bidhaa zote za ndege.
Uondoaji wa barafu kwenye uwanja wa ndege
Bila shaka usalama hupewa kipaumbele cha juu katika kila uwanja wa ndege. Hali za kusitishwa kwa shughuli zinazotokana na hali ya hewa zinaweza kuathiri uchumi na mseto wa hatua za uzuiaji na uondoaji wa barafu ni muhimu hata kwa ajili ya sababu za kiuslama.
Gari la zimamoto la uwanja wa ndege
Kwa kawaida lina mfumo wa kuendesha magurudumu yote na injini thabiti ili kwenda kwa kasi ya juu zaidi kadri iwezekanavyo. kwa hivyo, gari hili linaweza kuendeshwa kutoka katika kituo hadi kwenye eneo la tukio la ajali kwenye barabara ya ndege kwa kasi ya juu zaidi kadri iwezekanavyo.
Kujaza mafuta kwenye ndege katika uwanja wa ndege
Malori ya kujaza mafuta yanahitajika katika ukubwa tofauti kulingana na ukubwa wa uwanja wa ndege, mchakato wa kujaza mafuta na aina ya ndege. Yanaweza kujaza mafuta idadi ya hadi ndege 100 kwa siku.
Usalama
Kuepuka ajali na matukio bila shaka ni suala linalopewa kipaumbele cha juu katika viwanja vyote vya ndege duniani kote, hali inayomaanisha kuwa magari ya kutoa huduma yanahitaji kuwa salama na katika hali nzuri ya kutumika. Vifaa vya usalama kama vile mifuko ya hewa na mifuko ya hewa ya pazia, kati ya vitu vingine, ni vifaa muhimu.
Wakati wa kufanyakazi
Kasi, utendaji bora na usahihi ni muhimu katika huduma za usaidizi za uwanja wa ndege na ni muhimu kupatikana kwa wakati unaofaa. Hakuna nafasi kwa gari kutopatikana bila kutarajiwa. Hii inahitaji gari kupatikana kila wakati na kupanga mapema shughuli za matengenezo na ukarabati.
Tija
Pindi baada ya ndege kuwasili langoni, huzingirwa na magari mbalimbali maalum. Ufanisi na utendaji bora ni muhimu kwa ajili ya kutoa huduma bora. Kushughulikia ndege kwa kuweza kuona vizuri na usukani uliokazwa vizuri, ni baadhi ya vigezo ambavyo ni muhimu kwa utendaji bora zaidi.
Suluhu za huduma
Kampuni ya Scania husaidia kuhakikisha utendaji wako kwa kutoa huduma nyingi zilizobuniwa ili kufaa kwa kazi zako mahususi. Kitu chochote ambacho kinaweza kuboresha faida yako, utapata suluhu ya huduma ya Scania inayoishughulikia, kuanzia kwa ufadhili na kupata mafunzo ya udereva na huduma za ukarabati.
Huduma dijitali
Kutoa data kunatuwezesha kuunda huduma ambazo zinaweza kukupa thamani ya moja kwa moja ya biashara. Pata maelezo kuhusu jinsi unavyoweza kutumia huduma zetu dijitali na uchukue hatua katika shirika lako.
Ukarabati na matengenezo
Tunapanga mipango ya urekebishaji inayolingana na biashara yako, kuhakikisha muda wa kufanya kazi zaidi, kuongeza tija na kupunguza usumbufu katika utendakazi wako wa kila siku.
Gundua miundo ya malori ya Scania inayopendekezwa kwa uchukuzi katika uwanja wa ndege
Wasiliana nasi
Wasiliana nasi kwa njia inayokufaa, tafadhali teua chaguo lako hapa chini:
Badilisha upendavyo lori lako kwa uwezo bora
Tumia zana yetu ya usanidi iliyo rahisi kutumia ili ubadilishe upendavyo lori lako ili kuboresha tija na ufanisi. Jenga lori lako bora! Libadilishe liwe Scania.
Tafuta muuzaji aliyekaribu nawe
Wasiliana na wauzaji wetu walioidhinishwa ukiwa na maswali yoyote kuhusu bidhaa, huduma, au shughuli zetu katika eneo lako. Wasiliana nasi leo kwa msaada na usaidizi wa kitaalamu.