Chesisi ya Scania K- Travel
Sakafu ya juu
Mitambo ya injini
Chesisi ya Scania K yenye sakafu ya juu inapatikana ikiwa na aina mbalimbali za mitambo ya uendeshaji zilizo na ufanisi wa nishati na za kutegemewa zilizoboreshwa kwa trafiki ya umbali mrefu.
Injini | Nguvu inayotolewa | Toki | Udhibiti wa uchafuzi | Chaguzi za mafuta |
---|---|---|---|---|
Lita 9 | 320 Hp (235kW) | 1600 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Mota ya umeme | 130 kW | 1030 Nm | Hakuna uchafuzi | Umeme |
Giaboksi: Giaboksi ya kasi 12 na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania |
Ujazo | Nguvu inayotolewa | Toki | Udhibiti wa uchafuzi | Chaguzi za mafuta |
---|---|---|---|---|
Lita 9 | 320 Hp (235 kW) | 1600 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Lita 9 | 360 Hp (265 kW) | 1700 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Lita 13 | 370 Hp (272 kW) | 1900 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | HVO, Dizeli |
Lita 13 | 410 Hp (302 kW) | 2150 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Lita 13 | 450 Hp (331 kW) | 2350 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biodizeli, HVO, Dizeli |
Lita 13 | 500 Hp (368 kW) | 2550 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | HVO, Dizeli |
Ujazo wa mafuta (kiasi kinachoweza kutumika):
Lita 275 hadi 460
Giaboksi:
Giaboksi ya kasi 6 ya kiotomatiki kikamilifu
Giaboksi ya kasi 12 na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania
Chesisi ya sakafu ya juu na injini za pato za chini zinapatikana hapa chiniChesisi ya Mjini.
Injini | Nguvu inayotolewa | Toki | Udhibiti wa uchafuzi | Chaguzi za mafuta |
---|---|---|---|---|
Lita 9 | 340 Hp (250 kW) | 1600 Nm | Selective Catalytic Reduction (SCR) | Biogesi, Gesi asili |
Ujazo wa mafuta:
Lita 1260 - 1875 (CBG/CNG)
Lita 560–1120 (LBG/LNG)
Giaboksi:
Giaboksi ya kasi 6 ya kiotomatiki kikamilifu
Giaboksi ya kasi 12 na Mfumo wa Kubadilisha Gia Kiotomatiki wa Scania
Ekseli
Chesisi ya Scania yenye sakafu ya juu inapatikana katika anuwai kadhaa kuiwezesha kukidhi mahitaji tofauti ya uendeshaji.
4x2 - ekseli isiyodhibiti mzunguko wa magurudumu au ekseli inayodhibiti mzunguko wa magurudumu
6x2 - viangiko huru au ekseli iliyo imara
6x2*4 - ekseli isiyodhibiti mzunguko wa magurudumu au ekseli inayodhibiti mzunguko wa magurudumu
Kiwango cha sakafu
Njia ya kochi imepunguzwa, na kusababisha starehe ya juu ya abiria kupitia hatua chache kwenye ngazi, urefu kamili wa kusimama, na ufikiaji rahisi wa viti, bila kuathiri kiwango cha mizigo.
Vipengele vya muundo
Chesisi ya Scania K yenye sakafu ya juu inakidhi mahitaji ya waendeshaji katika kila bara. Kwa udhibiti kamili wa ubunifu na utengenzaji wa fremu na mfumo wa uendeshaji, kampuni ya Scania inatengeneza fremu za kutegemewa, za kudumu na za utendaji bora wa kipekee.
Ujenzi wa fremu ya chesisi
Ekseli ya mbele iliyoimarishwa inamaanisha kuwa uwezo wa mzigo umeongezeka kutoka tani 7.5 hadi 8.2. Pia huwezesha usambazaji wa uzani ulioboreshwa kati ya ekseli za mbele na za nyuma.
Teknolojia ya nguvu za injini
Mitambo ya uendeshaji vinavyotegemewa sana, vinavyodumu na vilivyo thabiti huwezesha kuokoa mafuta hadi 6% huku kuongezwa kwa udhibiti wa usafiri, na ubashiri unaoendelea na utendaji wa mipigo na utelezi, huchangia uokoaji zaidi.
Mfumo ya umeme
Usanifu mpya wa usambazaji wa nishati unakuja na vitengo vilivyoboreshwa vya udhibiti wa kielektroniki (ECUs) na utendaji ambao huboresha utendakazi na kuwezesha uchunguzi kwa ukarabati na matengenezo. Pia huwezesha utendakazi mpya ndani ya ADAS, uhamaji wa kielektroniki na mifumo ya usafiri unaojiendesha.
Vipengele vya usalama
Ili kuzuia ajali, makochi ya Scania yana mifumo na vipengele vya hali ya juu vya usalama. Mifumo hii humsaidia dereva kwa kuongeza ufahamu wao kwa watumiaji wa barabara wanaowazunguka au hata kusaidia kudhibiti gari inapohitajika. Udhibiti unaobadilika wa kasi ya usafiri wenye ubashiri amilifu, usaidizi wa kuweka Njia, onyo la mahali pasipoonekana, breki ya maegesho ya kielektroniki, onyo la kugongana na watumiaji wa barabara walio hatarini, ulinzi wa upande wa chini.
Eneo la dereva
Hutoa egonomiki bora kupitia paneli ya ala inayoweza kubadilishwa, uwekaji wa swichi unaonyumbulika. Paneli ya ala iliyo chini zaidi huongeza mwonekano. Magari yana uwezaji wa hali ya juu wa kuendeshwa na yenye eneo kubwa la kugeuza, mifumo ya hali ya juu ya usaidizi wa madereva, na ushughulikiaji ulioboreshwa wa uendeshaji, usukani na breki. Pia, hutoa usalama ulioongezeka, mfumo bora wa hali ya hewa na mfumo mzuri wa kupunguza kelele na mitikisiko.
Teknolojia ya viangiko vya mbele
Bila kuathiri uwezo wa kubeba abiria, viangiko vipya vya mbele kwa kujitegemea hutoa starehe bora ya abiria na kuongeza uwezo wa mzigo.
Toleo la bidhaa
Wasiliana na muuzaji wako
Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.