Usafirishaji wa mbao na bidhaa za misitu
Tunakusaidia ubadilishe upendavyo malori yako ya Scania ya usafirishaji wa bidhaa za misitu ili kuboresha uwezo na kurahisisha kazi yako.
Yameundwa kwa maisha ya msituni
Wakati sekta yako inahitaji kukabiliana na barabara mbaya na usafirishaji wa malighafi mchana na usiku, unahitaji magari yenye uwezo unaolingana na mahitaji yako ya biashara. Tumejitolea kubadilisha upendavyo gari lako kwa ukamilifu kabisa.
Yakuaminika na thabiti
Aina ya magari ya Scania XT yako tayari kukabiliana na changamoto ngumu zaidi. Yakiendeshwa na injini kuu ya V8, yameundwa kustahimili mazingira magumu, kupata muda wa kufanya kazi na kuongeza tija, ili uweze kuendesha shughuli zako kwa ufanisi.
Mbao
Ingawa wengine hufafanua changamoto za biashara zao kulingana na mzigo wa kulipiwa, ni barabara iliyo mbele yako inayokutambulisha. Kwa sababu kuna tofauti kubwa kati ya kuendesha gari kwenye barabara mbovu za msituni na kusafiri masafa marefu kwenye barabara kuu. Malori na huduma za Scania huja zikiwa zimeundwa kwa ajili ya biashara yako.
Usafirishaji wa mbao
Kuongezeka kwa tija kunategemea mzunguko wako na ubora wa barabara. Masafa mafupi mara nyingi humaanisha hali mbaya ya barabara na hutaka uthabiti. Ilhali masafa marefu yanahitaji gari lenye uzito ulioboreshwa, ambalo linaongeza kilo kadhaa kwenye mzigo wako wa kulipiwa. Hivi ndivyo unavyoweza kushughulikia mahitaji haya mawili, kibinafsi na kwa pamoja. Malori na huduma za Scania hukupa chaguo zote zinazokufaa.
Matumizi bora ya mafuta
Ili kuboresha kiwango cha tija yako na kupunguza gharama ya matumizi ya mafuta, Scania hujitahidi kila wakati kuboresha malori na huduma zetu. Kwa kuboresha mara kwa mara misingi mitatu ya kupunguza gharama ya mafuta - gari, dereva, huduma - tutasaidia biashara yako kustawi.
Wakati wa kufanyakazi
Neno wakati wa kufanyakazi linaweza kuonekana rahisi - lakini mtazamo mpana unaojumuisha huduma zote mbili zilizobinafsishwa, gari na dereva unahitajika ili kuufanikisha na kuudumisha. Kwa sababu ingawa maisha yako yote huenda hayategemei muda wa kufanya kazi- tofauti na madereva katika mfululizo wetu wa hali halisi "Hakuna Nafasi ya Kupumzika" - tuna uhakika kuwa biashara yako inategemea.
Tija
Katika Scania, tunaangazia biashara yako. Yote ni juu ya kuboresha tija, kuongeza urahisi wa ufikiaji na kupunguza muda unaohitajika ili kutekeleza shughuli husika. Kushiriki lengo sawa - kwamba biashara yako inapaswa kuwa na faida kadri iwezekanavyo.
Suluhu za huduma
Kampuni ya Scania husaidia kuhakikisha utendaji wako kwa kutoa huduma nyingi zilizobuniwa ili kufaa kwa kazi zako mahususi. Kitu chochote ambacho kinaweza kuboresha faida yako, utapata suluhu ya huduma ya Scania inayoishughulikia, kuanzia kwa ufadhili na kupata mafunzo ya udereva na huduma za ukarabati.
Huduma dijitali
Kutoa data kunatuwezesha kuunda huduma ambazo zinaweza kukupa thamani ya moja kwa moja ya biashara. Pata maelezo kuhusu jinsi unavyoweza kutumia huduma zetu dijitali na uchukue hatua katika shirika lako.
Ukarabati na matengenezo
Tunapanga mipango ya urekebishaji inayolingana na biashara yako, kuhakikisha muda wa kufanya kazi zaidi, kuongeza tija na kupunguza usumbufu katika utendakazi wako wa kila siku.
Gundua miundo ya malori ya Scania inayopendekezwa kwa uchukuzi wa kilimo
-
-
R-mfululizo
Hakuna ukinzani - kebini ya R tofauti kivyake ni imara lakini ni kali zaidi kuliko hapo awali. Jitayarishe kugeuza vichwa na mwili huu wa riadha ambao hufafanua upya starehe katika uchukuzi wa muda mrefu. -
Mfululizo wa S
Mfululizo wa S huongeza dau katika starehe ya madereva wa masafa marefu. Gundua mambo ya ndani ambayo ni kimbilio la starehe, yenye sakafu bapa na maeneo ya kuhifadhia yaliyopanuliwa, imeundwa kutoa nafasi kubwa ya kuishi.
Wasiliana nasi
Wasiliana nasi kwa njia inayokufaa, tafadhali teua chaguo lako hapa chini:
Badilisha upendavyo lori lako kwa uwezo bora
Tumia zana yetu ya usanidi iliyo rahisi kutumia ili ubadilishe upendavyo lori lako ili kuboresha tija na ufanisi. Jenga lori lako bora! Libadilishe liwe Scania.
Tafuta muuzaji aliyekaribu nawe
Wasiliana na wauzaji wetu walioidhinishwa ukiwa na maswali yoyote kuhusu bidhaa, huduma, au shughuli zetu katika eneo lako. Wasiliana nasi leo kwa msaada na usaidizi wa kitaalamu.