Tanzania

Malori ya shughuli za uchukuzi wa rejareja, utarishi wa moja kwa moja na posta

Uwezo mkubwa wa upakiaji kutoka kituoni hadi ghalani

Beba zaidi, unapoenda huko na unaporudi- lengo daima ni uboreshaji kamili wa upakiaji. Lakini kwa ushindani mkali na faida ndogo, ni changamoto kubwa. Scania hutoa suluhu zilizoundwa mahususi ambazo hukuletea matokeo bora kila wakati.

 

Wewe ni muhimu kwa mkondo wa usambazaji. Na wakati mtu mwingine anasubiri kuchukua mzigo wako, huwezi kumudu kuchelewa - au kutokuwa kazini Tunajua kuwa biashara yako ni ya barabarani.  

Gundua malori ya shughuli za uchukuzi wa rejareja, utarishi na posta

Matumizi bora ya mafuta

Ili kuboresha kiwango cha tija yako na kupunguza gharama ya matumizi ya mafuta, Scania hujitahidi kila wakati kuboresha malori na huduma zetu. Kwa kuboresha mara kwa mara misingi mitatu ya kupunguza gharama ya mafuta - gari, dereva, huduma - tutasaidia biashara yako kustawi.

Wakati wa kufanyakazi

Neno wakati wa kufanyakazi linaweza kuonekana rahisi - lakini mtazamo mpana unaojumuisha huduma zote mbili zilizobinafsishwa, gari na dereva unahitajika ili kuufanikisha na kuudumisha. Kwa sababu ingawa maisha yako yote huenda hayategemei muda wa kufanya kazi- tofauti na madereva katika mfululizo wetu wa hali halisi "Hakuna Nafasi ya Kupumzika" - tuna uhakika kuwa biashara yako inategemea.

Tija

Katika Scania, tunaangazia biashara yako. Yote ni juu ya kuboresha tija, kuongeza urahisi wa ufikiaji na kupunguza muda unaohitajika ili kutekeleza shughuli husika. Kushiriki lengo sawa - kwamba biashara yako inapaswa kuwa na faida kadri iwezekanavyo.

Suluhu za huduma

Kampuni ya Scania husaidia kuhakikisha utendaji wako kwa kutoa huduma nyingi zilizobuniwa ili kufaa kwa kazi zako mahususi. Kitu chochote ambacho kinaweza kuboresha faida yako, utapata suluhu ya huduma ya Scania inayoishughulikia, kuanzia kwa ufadhili na kupata mafunzo ya udereva na huduma za ukarabati.

Huduma dijitali

Kutoa data kunatuwezesha kuunda huduma ambazo zinaweza kukupa thamani ya moja kwa moja ya biashara. Pata maelezo kuhusu jinsi unavyoweza kutumia huduma zetu dijitali na uchukue hatua katika shirika lako.

Ukarabati na matengenezo

Tunapanga mipango ya urekebishaji inayolingana na biashara yako, kuhakikisha muda wa kufanya kazi zaidi, kuongeza tija na kupunguza usumbufu katika utendakazi wako wa kila siku.

Wasiliana nasi

Wasiliana nasi kwa njia inayokufaa, tafadhali teua chaguo lako hapa chini: 

Badilisha upendavyo lori lako kwa uwezo bora

Tumia zana yetu ya usanidi iliyo rahisi kutumia ili ubadilishe upendavyo lori lako ili kuboresha tija na ufanisi. Jenga lori lako bora! Libadilishe liwe Scania. 

Tafuta muuzaji aliyekaribu nawe

Wasiliana na wauzaji wetu walioidhinishwa ukiwa na maswali yoyote kuhusu bidhaa, huduma, au shughuli zetu katika eneo lako. Wasiliana nasi leo kwa msaada na usaidizi wa kitaalamu.