Procare
Gari Kutumika kwa Muda Uliowekwa
Scania ProCare ni huduma mpya maalum ya matengenezo ya magari kutoka Scania, ambayo inaondoa kabisa hatari ya gari lako kukumbwa na hitilafu zisizotarajiwa. Kwa shughuli ambapo muda wa usafirishaji na muda uliowekwa wa kutumika kwa gari ni muhimu zaidi katika kudumisha uaminifu, Huduma ya Scania ProCare inaweza kuhakikisha kuwa gari lako linatumika kwa muda uliowekwa.
Ikiwa imebuniwa kwa msingi wa Matengenezo Rahisi ya Scania (Scania Flexible Maintenance), huduma ya Scania ProCare inatumia mseto wa mbinu za matengenezo rahisi na matengenezo yasiyokatiza shughuli ya wakati ambapo gari halitumiki na kufanya ukaguzi wa mapema wa hali ya gari na ufuatiliaji wa hali ya gari kila wakati. Hii inajumuisha kufanya mabadiliko ya sehemu za gari kwa ajili ya uzuiaji wa hitilafu kabla hazijasababisha kukatizwa kwa shughuli zako – hatua ambayo inadumisha lori la Scania barabarani kwa muda mrefu kadri linavyozidi kutumika.
Huduma maalum ya matengenezo
Tunaboresha zaidi huduma ya matengenezo ya Scania, huduma ya Scania ProCare ni huduma maalum ya matengenezo ya gari kwa magari yote ya Scania yaliyotengenezwa kuanzia mwaka wa 2019 na kuendelea – kuanzia kwa magari mengi ya kimataifa hadi kwa mikataba ya magari ya binafsi.
Kama huduma maalum iliyounganishwa, Scania itadhibiti pia mpango wa matengenezo kwa ajili yako, kwa kutumia mbinu ya uchunguzi wa data na kuendelea kufuatilia hali ya gari lako na kukufahamisha iwapo umefika muda wa kuweka mpango wa kufanya matengenezo. Kwa nfano, ingawa hitilafu kubwa ya injini inaweza kusababisha gari lako kutotumiwa kwa siku kadhaa, sababu ya msingi iliyosababisha hitilafu husika inaweza kusuluhishwa kwa masaa kadhaa tu kwa kutumia huduma ya Scania ProCare. Hatua hii haikupi tu utulivu wa mawazo, lakini pia inakuruhusu uangazie zaidi suala muhimu – kuhusu shughuli zako.
Huduma bora ya matengenezo ya kuzuia hitilafu
Ukiwa na mkataba wa huduma ya ProCare, gari lako la Scania lililounganishwa litaendelea kuripoti hali yake ya kiufundi moja kwa moja kwa Scania katika wakati halisi. Kwa kuunganisha data ya gari lako na data ya kina na maalum ya uchunguzi wa utendekazi ya Scania – iliyokusanywa kwa miaka mingi – Scania itatambua na kubainisha mapema na kusuluhisha mapema hitilafu zozote zinazoweza kusababisha kuharibika kwa gari kabla hazijaanza kuathiri shughuli zako.
Wasiliana na muuzaji wako
Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.