Magari ya kazi
Uthabiti kwa ajili ya mandhari na kazi zote
Iwe unafanya kazi katika maeneo ya mashambani, karibu na vikundi vya migodi au katika mgodi mkuu, kudumisha upatikanaji wa wafanyakazi na vifaa na kudumisha hali nzuri ya barabara ni muhimu katika kuboresha matokeo ya utendakazi.
Si lori lolote tu
Kundi kikubwa cha malori ya kazi ni msingi wa usalama wa mgodi na katika kupunguza muda wa mapumziko na kusimamishwa kwa kazi. Malori ya kazi za kampuni ya Scania yamebuniwa kuwa rahisi kuendeshwa katika hali ngumu zaidi ili kusaidia kusafirisha wafanyakazi, vifaa na bidhaa nyingine muhimu ambazo unahitaji kwa kazi yako.
Uwezo wa kukarabati
Katika migodi, athari za kukosa mafuta au huduma za ukarabati zinazoweza kupatikana kwa haraka zitaathiri utendaji na kusababisha gharama ambazo hazikutarajiwa. Ikijumuisha gharama za uzalishaji. Wakati mashine za kuchimbua zenye uzito wa tani 360 zinahitaji kuwekwa mafuta, kila dakika muhimu katika kudumisha uzalishaji. Malori ya kazi ya kampuni ya Scania yatakuwepo na kukamilisha kazi bila matukio ya ucheleweshaji yanayosababisha hasara.
Endelea kufanya kazi baada ya muda mfupi
Ukarabati na matengenezo bora ni muhimu katika kudumisha utendakazi wa mashine. Kutokana na muundo rahisi wa kukarabatiwa kwa malori ya kampuni ya Scania na upatikanaji wa vipuri kwa urahisi, ukarabati utachukua muda mchache zaidi. Hivyo ndivyo sisi hufanikiwa kurejesha malori kazini haraka iwezekanavyo. Njia bora ya kupunguza gharama.
Usalama ni muhimu
Katika kampuni ya Scania, usalama umepewa kipaumbele cha juu. Malori yetu hujaribiwa kwa kina zaidi ili kutimiza viwango vikali zaidi vya usalama duniani. Kuanzia kwa chumba cha dereva ambacho kimetengenezwa kwa kizimba imara cha chuma, hadi katika mifumo inayotumika ya usalama, malori ya uchimbaji migodi ya kampuni ya Scania yamebuniwa kuhakikisha usalama wa kiwango cha juu kutoka katika kila pembe.
Zimebuniwa kwa ajili ya kutumiwa kwa urahisi zaidi
Kusawazisha mahitaji ya kupunguza gharama na utendaji na masuala ya uzito na kubadilishwa ili kufaa kwa kazi mahususi kumesababisha kutungwa kwa moduli ya maalum ya mafunzo ya kampuni ya Scania. Kwa sasa kampuni ya Scania inatoa vifaa thabiti na vya kutegemewa vinavyofaa kwa kazi yako.
Mzigo
Nafasi kati ya fremu ya gari na barabara Lori la kampuni ya Scania lenye sehemu ya chini iliyoinuka juu zaidi lina nafasi kubwa kati ya fremu ya gari na barabara.
Fremu
Kutokana na uzoefu wa miaka mingi, aina ya fremu za wastani za malori ya kampuni ya Scania inatoa fursa nyingi zaidi za kubadilishwa. Fremu zilizoungwa na fremu moja moja za nguvu mbalimbali.
Injini
Njia bora ya kuboresha uchumi wa uendeshaji ni kutafuta usawa bora zaidi kati ya hali ya kuendeshwa, hali ya kuanzisha na matumizi ya mafuta. Tunafanya hivyo kwa kuboresha mfumo wote wa uendeshaji.
Wasiliana na muuzaji wako
Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.
Ikiwa na chaguo nyingi mno na mpangilio wa mipangilio ya wastani, unaweza kuweka mipangilio inayokufaa kwenye lori lako. Ifanye iwe Scania.