Kazi ya uchimbaji migodi
Yanafaa kwa kazi ngumu ya uchimbaji migodi
Jambo muhimu zaidi katika shughuli za uchimbaji migodi ni kuzoa vitu vingi zaidi kadri iwezekanavyo kwa gharama ya chini zaidi. Kitu chochote na hali yoyote, magari yetu yamebuniwa kufanya kazi hata katika mazingira mabaya zaidi ya ndani ya migodi. Mahali popote duniani.
Yamebuniwa kufanya kazi kwa muda mrefu
Malori ya kampuni ya Scania ya kufanya kazi ndani ya migodi yamebuniwa kutimiza masharti ya kiwango cha juu zaidi kwa ufanisi wa kiwango cha juu zaidi kadri iwezekanavyo. Kwa kuchanganua kwa makini mzunguko wa shughuli zako, tunaweza kubadilisha malori ili kutengeneza malori yanayofaa kwa kutoa huduma bora zaidi.
Mambo madogo huchangia mambo makubwa
Jambo la msingi katika kutengeneza faida kutokana na kazi ya uchimbaji migodi inahusu kudhibiti pesa na gharama za shughuli. Ni muhimu kuangalia bidhaa zetu. Mara nyingi gharama ya jumla ya chini ya matumizi ya magari yetu inashinda faida ya kutumia kifaa kikubwa cha kawaida cha uchimbaji migodi. Malori thabiti na ya kutegemewa ya kampuni ya Scania ni chaguo bora zaidi ya magari ya kutumika katika kazi ngumu zaidi ya uchimbaji migodi.
Endelea kufanya kazi baada ya muda mfupi
Ukarabati na matengenezo bora ni muhimu katika kudumisha utendakazi wa mashine. Kutokana na muundo rahisi wa kukarabatiwa kwa malori ya kampuni ya Scania na upatikanaji wa vipuri kwa urahisi, ukarabati utachukua muda mchache zaidi. Hivyo ndivyo sisi hufanikiwa kurejesha malori kazini haraka iwezekanavyo. Njia bora ya kupunguza gharama.
Usalama ni muhimu
Katika kampuni ya Scania, usalama umepewa kipaumbele cha juu. Malori yetu hujaribiwa kwa kina zaidi ili kutimiza viwango vikali zaidi vya usalama duniani. Kuanzia kwa chumba cha dereva ambacho kimetengenezwa kwa kizimba imara cha chuma, hadi katika mifumo inayotumika ya usalama, malori ya uchimbaji migodi ya kampuni ya Scania yamebuniwa kuhakikisha usalama wa kiwango cha juu kutoka katika kila pembe.
Yametengenezwa ili kudumu kwa muda mrefu
Katika kampuni ya Scania tunatengeneza gari lako ili lidumu kwa muda mrefu na kupunguza gharama ya jumla ya matumizi. Tunatoa aina nyingi za fremu za magari, mifumo ya kusambaza nishati na ekseli, ambayo inaweza kuwekwa ili kutimiza mahitaji yako mahususi.
Mzigo
Unapohitaji kupunguza uzito shehena ya kulipiwa, chaguo ni rahisi. Kampuni ya Scania inatengeneza malori mepesi zaidi yanayopatikana sokoni. Ingawa bado ni ya kutegemewa na thabiti zaidi. Yanayofaa zaidi kwa utendaji. Yanafaa zaidi kwa kazi.
Fremu
Kutokana na uzoefu wa miaka mingi, aina ya fremu za wastani za malori ya kampuni ya Scania inatoa fursa nyingi zaidi za kubadilishwa. Fremu zilizoungwa na fremu moja moja za nguvu mbalimbali.
Injini
Utoaji wa nishati ya kiwango cha juu na matumizi bora zaidi ya mafuta ni baadhi ya manufaa ya injini maarufu za kampuni ya Scania. Aina nyingi zinapatikana ambazo zinatoa nishati ya hadi ya 730 hp. Kwa kuwepo kwa aina nyingi za injini, giaboksi na gia zetu za katikati, unaweza kubainisha lori ambalo linafaa zaidi kwa kazi yako ya uchimbaji migodi.
Wasiliana na muuzaji wako
Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.
Ikiwa na chaguo nyingi mno na mpangilio wa mipangilio ya wastani, unaweza kuweka mipangilio inayokufaa kwenye lori lako. Ifanye iwe Scania.