Usafiri katika uwanja wa ndege
Kwa wakati unaofaa
Na ratiba yenye shughuli nyingi
Ingawa siku zako za kukaa katika uwanja wa ndege zinaweza kutofautiana, kuna hali za utofauti ambazo zinafanana. Hitaji la kutunza mazingira na urahisi wa kubadilika pamoja na ratiba yenye shughuli nyingi. Kwa bahati nzuri, urahisi wa kubadilisha shughuli zetu ni kitu tunachothamini katika kampuni ya Scania. Kwa kutumia mfumo wetu unaoweza kubadilika kama rasilimali yetu kuu zaidi, tunaweza kutengeneza bidhaa za kufaa karibu kazi yoyote. Ikiwa ni pamoja na yako.
Kufagia barabara ya ndege
Kwa kutegemea ukubwa na wingi wa shughuli, uwanja wa ndege unaweza kuwekewa vifagio vikubwa mahususi vya kufagia barabara ya ndege na vifagio vidogo zaidi vya kufagia maeneo ya teksi na huduma.
Huduma ya uchukuzi wa chakula katika uwanja wa ndege
Malori ya uchukuzi wa chakula yanapatikana katika ukubwa tofauti na yanaweza kuwekewa vyumba vidogo vyenye halijoto zinazodhibitiwa. Utendaji huongezwa ikiwa lori linaweza kubeba bidhaa zote za ndege.
Uondoaji wa barafu kwenye uwanja wa ndege
Bila shaka usalama hupewa kipaumbele cha juu katika kila uwanja wa ndege. Hali za kusitishwa kwa shughuli zinazotokana na hali ya hewa zinaweza kuathiri uchumi na mseto wa hatua za uzuiaji na uondoaji wa barafu ni muhimu hata kwa ajili ya sababu za kiuslama.
Gari la zimamoto la uwanja wa ndege
Kwa kawaida lina mfumo wa kuendesha magurudumu yote na injini thabiti ili kwenda kwa kasi ya juu zaidi kadri iwezekanavyo. kwa hivyo, gari hili linaweza kuendeshwa kutoka katika kituo hadi kwenye eneo la tukio la ajali kwenye barabara ya ndege kwa kasi ya juu zaidi kadri iwezekanavyo.
Kujaza mafuta kwenye ndege katika uwanja wa ndege
Malori ya kujaza mafuta yanahitajika katika ukubwa tofauti kulingana na ukubwa wa uwanja wa ndege, mchakato wa kujaza mafuta na aina ya ndege. Yanaweza kujaza mafuta idadi ya hadi ndege 100 kwa siku.
Usalama
Kuepuka ajali na matukio bila shaka ni suala linalopewa kipaumbele cha juu katika viwanja vyote vya ndege duniani kote, hali inayomaanisha kuwa magari ya kutoa huduma yanahitaji kuwa salama na katika hali nzuri ya kutumika. Vifaa vya usalama kama vile mifuko ya hewa na mifuko ya hewa ya pazia, kati ya vitu vingine, ni vifaa muhimu.
Wakati wa kufanyakazi
Kasi, utendaji bora na usahihi ni muhimu katika huduma za usaidizi za uwanja wa ndege na ni muhimu kupatikana kwa wakati unaofaa. Hakuna nafasi kwa gari kutopatikana bila kutarajiwa. Hii inahitaji gari kupatikana kila wakati na kupanga mapema shughuli za matengenezo na ukarabati.
Tija
Pindi baada ya ndege kuwasili langoni, huzingirwa na magari mbalimbali maalum. Ufanisi na utendaji bora ni muhimu kwa ajili ya kutoa huduma bora. Kushughulikia ndege kwa kuweza kuona vizuri na usukani uliokazwa vizuri, ni baadhi ya vigezo ambavyo ni muhimu kwa utendaji bora zaidi.
Suluhisho za Huduma
Kampuni ya Scania husaidia kuhakikisha utendaji wako kwa kutoa huduma nyingi zilizobuniwa ili kufaa kwa kazi zako mahususi. Kitu chochote ambacho kinaweza kuboresha faida yako, utapata huduma ya kampuni ya Scania inayokishughulikia, kuanzia kwa ufadhili na kupata mafunzo ya udereva na huduma za ukarabati.
Wasiliana na muuzaji wako
Tafadhali wasiliana nasi ikiwa una maswali yoyote kuhusu bidhaa au huduma zetu au shughuli nyingine zinazotekelezwa katika kampuni ya Scania.
Ikiwa na chaguo nyingi mno na mpangilio wa mipangilio ya wastani, unaweza kuweka mipangilio inayokufaa kwenye lori lako. Ifanye iwe Scania.