Matumizi bora ya mafuta
Fuata kiongozi
TUNAZINGATIA VIPENGELE VYOTE KUHUSIANA NA SUALA LA KUBORESHA MATUMIZI YA MAFUTA
Katika kampuni ya Scania, uboreshaji ni mchakato wa kufanya maboresho mara kwa mara. Katika sekta ya kuboresha matumizi ya jumla ya nishati, tunashughulikia kila kipengele. Matokeo yake huwa bora zaidi. Teknolojia iliyoboreshwa ya kutengeza injini, kutovuta hewa kwa wingi na uthabiti wa kuzunguka vikiunganishwa na vifaa mahiri na zana muhimu, vinasadia gari lako kutumia mafuta kwa njia bora zaidi, bila kujali shughuli zako.
Elimu mwendo
Katika kampuni ya Scania, ubunifu wa magari ni mchakato endelevu. Magari yaliyoshinda tuzo yanayopatikana leo ni matokeo ya karibu karne moja ya kufanya uhandisi kwa umakini na kuboresha hata vipengele vidogo zaidi vya elimu mwendo na hali na ufanisi wa wafanyakazi. Hakuna kipengele chochote ambacho hakijashughulikiwa katika mchakato wa kutengeneza gari bora zaidi, kuanzia kwa sehemu ya boneti ya kupitisha hewa hadi kwa taa za nyuma ya gari. Isitoshe, hata sehemu ya chini ya gari imeboreshwa ili kupunguza hali isiyotakikana ya kudhibitiwa na hewa kujikokota.
TEKNOLOJIA YA INJINI
Teknolojia ya injini ya mwako wa ndani ya kampuni ya Scania imebuniwa ili kuboresha matumizi ya mafuta ya gari lako, kupunguza utoaji wa gesi ya kaboni na kutoa nishati ya kiwango cha kutosha. Tunajivunia zaidi lengo letu la kuwa mbele hatua moja kila wakati kuhusiana na suala la teknolojia ya injini na tunatengeneza vijenzi vyote muhimu ndani ya kampuni yetu.
OKOA 10% YA GHARAMA YA MAFUTA
Punguza kasi kutoka 90 km/h hadi 80 km/h.
LENGO: KUENDESHA GARI BILA KUTUMIA MAFUTA KWA 20% YA SAFARI
Okoa mafuta kwa kuendesha gari bila kutumia mafuta kwa 20% ya kila safari ndefu.
HUDUMA ZA UKARABATI WA KITAALAMU
Ulainishaji wa ekseli, presha ya magurudumu, urekebishaji wa kizuia hewa – fanya gari lako liendelee kuboresha matumizi ya mafuta kadri iwezekanavyo kwa kutumia huduma za ukarabati wa kitaalamu za kampuni ya Scania.
MFUMO WA KUKADIRIA MATUMIZI YA MAFUTA KWENYE MTEREMKO
Mfumo wa Kubashiri Mapema hutumia GPS ili kubashiri mandhari mapema na kurekebisha gia na kasi ya kuendesha ipasavyo. Kwa kufanya ubashiri bora kila wakati, hali hii imethibitishwa kumpa dereva wako usaidizi wa kutosha na kuokoa hadi 2% ya mafuta.
MFUMO WA KUBADILISHA GIA KIOTOMATIKI
Mfumo huu wa kiotomatiki wa kubadilisha gia umethibitishwa kupunguza matumizi ya mafuta na kuboresha starehe ya dereva, hali ambayo inaondoa haja ya kukagua kasi na kubadilisha gia. Giaboksi ya mfumo wa kubadilisha gia kiotomatiki inatoa hali nne za utendaji (Kawaida, Bila kutumia mafuta, Nishati na Nje ya barabara) na inasaidia madereva kuzingatia mazingira yao.
USAIDIZI WA DEREVA
Mfumo wa moja kwa moja ambao unawapa madereva wako majibu ya papo hapo kuhusu usalama na matumizi ya mafuta pamoja na muhtasari kamili baada ya kazi kukamilika.
LINDA RASILIMALI YAKO MUHIMU ZAIDI
Madereva wako ni rasilimali muhimu zaidi katika kuboresha matumizi ya mafuta na kupunguza muda wa mapumziko. Kwa kuzingatia jambo hili, tumebuni mfululizo wa huduma na zana za kuwasaidia. Ukufunzi na Mafunzo ya Dereva wa Scania yamethibitishwa kuwa na manufaa kwa madereva wapya na wenye uzoefu na yanaweza kubuniwa ili yafae mahitaji yako mahususi.
UKUFUNZI NA MAFUNZO YA DEREVA
Yakiwa na sehemu mbalimbali za kuangazia, Mafunzo ya Dereva wa Scania na Ukufunzi wa ziada husaidia madereva wako kutenda kazi kwa kiwango cha juu zaidi, hali ambayo inasababisha kuongezeka kwa usalama wa barabarani, kuboresha matumizi ya mafuta na kupunguza uchafuzi wa mazingira.
ZANA YA UKADIRIAJI WA DEREVA
Ufuatiliaji na kupata majibu ni muhimu katika kutambua na kulenga sehemu zinazoweza kuboreshwa katika mtindo wa uendeshaji. Zana ya Ukadiriaji wa Dereva huchanganua na kulinganisha kila safari na safari nyingine zilizofanywa na madereva katika hali zinazofanana. Kisha mtindo wa uendeshaji hukadiriwa kulingana na vigezo kama vile kuendesha polepole, kuendesha bila kutumia mafuta na matarajio, ambavyo humpa dereva wako majibu ya jinsi ya kujiboresha kupitia Programu ya Kudhibiti Magari ya Kazi na kwenye tovuti ya mtandaoni.